• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

VIJANA WATAKIWA KUPATA ELIMU YA AFYA YA UZAZI, ZINAZOTOLEWA KWENYE VITUO VYA AFYA ARUSHA DC.

Posted on: August 24th, 2019

Na. Elinipa Lupembe.

Vijana katika Halmashauri ya Arusha, Wilaya ya Arumeru, wametakiwa kuhudhuria kwenye Vituo Vya Afya, kupata mafunzo Afya ya uzazi na Uzazi wa mpango kupitia Huduma Rafiki kwa Vijana, huduma inayotolewa kupitia Mradi wa Tupange pamoja, mradi unaotekelezwa na halmshauri, kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la JHPIEGO.

Rai hiyo imetolewa na Mratibu wa Shirika la JHPIEGO Mkoa wa Arusha, Waziri Njau, katika semina ya mafunzo ya Afya ya Uzazi kwa vijana kupitia Huduma Rafiki kwa Vijana, mafunzo yaliyofanyika kwenye Ofisi ya Kata ya Moivo, mwishoni mwa wiki iliyopita.

Njau amesema, kwa kawaida, elimu ya Afya ya Uzazi na Uzazi wa mpango, hubadilika kutokana na tafiti mbalimbali zinaendelea kufanywa na wanasayansi, hivyo ni vyema kuhudhuria mafunzo hayo, mara kwa mara ili kufahamu zaidi juu ya afya ya Uzazi na uzazi salama.

"Elimu ya Afya ya Uzazi, iliyotolewa zamani ni tofauti na elimu ya sasa kutokana, maendeleo ya sayansi na teknolojia, yamesababisha kugundulika kwa dawa na vimelea mbalimbali ambavyo hapo awali havijulikani" amesema Njau

Naye Mratibu wa Tupange pamoja kata ya Moivo, Kylie Gyubi, amesema vijana wanapaswa kujitambua na kutambua afya zao, kwa kutembelea vituo vya Afya na kukutana na wataalamu wa afya ya uzazi salama ili kupima na kupata ushauri juu ya Afya ya uzazi.

"Vijana wengi wamekuwa wakitumia njia za uzazi wa mpango bila kufuata ushauri wa wataalam wa afya, jambo linawasababisha kupata madhara kiafya na kudhani kuwa njia hizo sio salama, kumbe tatizo ni taarifa zisizo sahihi juu ya dawa hizo" amesema Gyubi

Hata hivyo vijana hao wamekiri kuwa na taarifa zaidi za Uzazi wa Mpango kuliko afya ya Uzazi, kutokana na ukweli kwamba mara nyingi, huduma hiyo hutolewa kwa vijana ambao tayari wamepata watoto na kuanza kuhudhuria kliniki.

Wamethibitisha kufuta ujinga nje ya shule, kutokana na elimu waliyoipata iliyowawezesha kufahamu kuwa, afya ya uzazi ni zaidi ya uzazi wa mpango, inayomuwezesha kijana kutambua mabadiliko ya mwili wake, jinsi ya kuishi na kuyamudu mabadiliko hayo, kujikinga na mimba za utotoni, mimba zisizotarajiwa bila kutumia dawa zisizo rasmi, kujiandaa kwa ajili ya kuanzisha familia pamoja na kujikinga na magonjwa yanayotokana na ngono zembe hasa gonjwa hatari la UKIMWI.

Kijana Juma Saidi, amesema kuwa  kutokana na ukosefu wa taarifa sahihi za afya ya uzazi kwa vijana, vijana wengi wamejikuta wakiingia kwenye mgogoro wa malezi ya watoto bila kujipanga, huku wasichana wakikatiza masomo kwa ajili ya mimba, kutokana na uelewa mdogo juu ya afya ya uzazi kwa vijana.

"Vijana wengi wamejikuta wanalazimika kuoana kwa kuwa tayari wameshapeana mimba,  na kuanza majukumu ambayo hawakuwa wamejipanga jambo ambalo, linasababisha ndoa hizo kuvunjika na kuingia kwenye migogoro mikubwa na kuwa na ongezeko kubwa la watoto wa mitaani" amesema kijana huyo.

Aidha Said ameongeza kuwa, vijana wengi hufundishana wenyewe na kuanza kujamiiana, huku wengi wakuamini kuwa, ukimuandaa msichana vizuri, na kujamiiana ndani ya dakika tano, hawezi kupata maambukizi ya UKIMWI, taarifa ambayo si za kweli, tendo la kujamiiana linaweza kuambukiza magonjwa ya ngono, kansa ya shingo ya kizazi na ugonjwa wa UKIMWI.

Naye Raja Matela licha ya kuishukuru timu ya Tupange Pamoja kwa kuwapatia elimu hiyo, ameiomba timu hiyo kuendelea kutoa elimu hii kwa jamii, ili kubadili mtazamo hasi na kuwafanya kuwa mabalozi wazuri katika kuhamasisha Afya ya uzazi na Uzazi wa mpango na Huduma Rafiki kwa Vijana,. kwani itasaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto na kuwa na uzazi salama.

"Kabla ya kupata elimu hii tulikuwa tunafahamu kuwa unapotumia njia za uzazi wa mpango kwa mwanamke huharibu umbile lake lakini kasasa tumegundua si kweli kwamba njia za uzazi wa mpango haziwezi kuharibu umbile la mwanamke" amesema kijana huyo

Afisa Vijana, halmashauri ya Arusha, Ahadi Mlai, amewataka vijana hao, kukutana kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi, ili kujifunza na kuongeza maarifa juu ya Afya ya uzazi na Uzazi wa mpango, na kuongeza kuwa kwa sasa 'Huduma Rafiki kwa Vijana', imeanza kutolewa kwenye vituo 15 vya  kutolea huduma za Afya, ndani ya hamashauri hiyo na kuwasisitiza vijana, kufika kwenye vituo hivyo kupata taarifa sahihi juu ya Afya ya Vijana.

Mradi wa Tuwavushe salama hutoa fursa kwa vijana  kujiongezea maarifa, uelewa, ujuzi na mbinu juu ya Afya uzazi na Uzazi wa mpango kwa kutumia njia salama zitakazo punguza vifo vya mama na mtoto.


Vijana wa kata ya Moivo, wakisikiliza mafunzo ya elimu ya Afya ya Uzazi kwa vijana, kwenye ofisi ya kata ya Moivo.

Mratibu wa Tupange pamoja kata ya Moivo, Kylie Gyubi, akifundisha vijana njia ya asili ya uzazi wa mpango kwa kutumia zana halisi.


Mratibu wa Shirika la JHPIEGO Mkoa wa Arusha, Waziri Njau, akitoa mada kwa vijana, juu ya Afya ya Uzazi na Uzazi wa mpango kwa vijana.

Vijana wakiendelea na mafunzo


Afisa Vijana, halmadhauri ya Arusha, Ahadi Mlai, akitoa mada wakati wa mafunzo ya Afya ya Uzazu na uzazi wa mpango kwa vijana.





Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.