• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

VIJANA WATAKIWA KUFAHAMU 4% YA MIKOPO YA VIJANA INAYOTOLEWA NA SERIKALI NI FURSA NA SIO ZAWADI

Posted on: August 21st, 2020

Na. Elinipa Lupembe.

       Vijana wametakiwa kutambua kuwa, mikopo ya asilia 4 inayotolewa na serikali ni fursa na sio zawadi, bali ni fedha zinazotolewa  kwa ajili ya kuendesha biashara na kujiimarisha kiuchumi, kwa maendeleo binafsi ya kijana, familia zao na taifa kwa ujumla.

   Hayo yameelezwa na Afisa Maendeelo ya Jamii, halmashauri ya Arusha, Angela Mvaa, alipofungua mafunzo kwa vijana juu asilimia 4 ya mikopo ya vijana inayotolewa na serikali, misingi ya kuanzisha na kuendesha biashara na masoko, mafunzo yaliyotolewa  na shirika la Vision for Youth la Jijinj Arusha, kwenye ukumbi wa mikutano, halmashauri ya Arusha.

    Afisa Maendeleo huyo, amewasisitiza vijana hao, kutambua kuwa, serikali iliamua kutumia kodi za watanzania kutoa mikopo hiyo kwa vijana kutokana na uhaba wa ajira nchini na duniani, ili  kuwawezesha vijana kujiajiri kwa kufanya biashara za mitaji midogo, kufuatia fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye maeneo yao, sambamba na kukuza mitaji kuelekea uchumi wa viwanda.

     Amesema kuwa licha ya vijana wengi sasa, kuwa na mwamko chanya na kuchukua mikopo hiyo, tofauti na miaka ya nyuma, lakini bado kuna changamoto ya baadhi ya vijana kishindwa kurejesha mikopo hiyo kwa wakati, kutokana na kuchukua fedha, bila ya kuwa na malengo thabiti, na kujikuta wakitumia fedha hizo kwa matumizi binafasi, jambo linalokwamisha ukuaji wa mitaji na wakati mwingine vikundi kufa.

     "Niwasihi vijana kutambua, fedha manazokopeshwa sio zawadi, ni fedha za kuafanyia biashara na kukuza mitaji yenu na si vinginevyo, tumieni fedha hizo kulingana na biashara na shughuli mlizokusudia kufanya kupita maandiko yenu ya miradi wakati wa kuomba mkopo, fuateni maelekezo ya uendeshaji wa biashara yanayotolewa kabla ya kupata mikopo, ili muweze kurejesha fedha hizo na kufikia lengo la serikali" amesisitiza Afisa Maendeleo huyo

      Aidha Afisa Maendeleo huyo ameweka wazi mafanikio makubwa  ya serikali ya awamu ya tano katika utoaji wa mikopo kwa vijana, licha ya changamoto zinazowakabili baadhi ya vijana, lakini kwa sasa vijana wameanza kupata mwamko na uelewa juu ya vikundi na mikopo hiyo, na kuongeza kuwa, kwa kipindi cha miaka mitano, halmashauri ya Arusha imefanikiwa kukopesha vijana 522 kwenye vikundi 10 na jumla ya shilingi milioni 280 zilikopeshwa kwa vikundi hivyo vya vijana..

     Hata hivyo, vijana hao wamekiri kuwa na changamoto ya urejeshaji kwa baadhi ya wanavikundi wenzao lakini changamoto hizo zinaendelea kupungua, kutokana na ufuatiliaji wa karibu pamoja na mafunzo wanayopopewa mara kwa mara na serikali kwa kushirikiana na  wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali, jambo ambalo limeanza kuzaa matunda kwa vijana wengi sasa.

  Mwenyekiti wa kikundi cha Unguuni Youth Group kilichopo kijiji cha Nduruma, licha ya kuishukuru serikali kwa kuwakomboa vijana kiuchumi, amekiri kuwa, awali vijana walikuwa wanachangamoto nyingi, zilizosababishwa na uelewa mdogo juu ya vikundi na uendeshaji wa biadhara, lakini mafunzo na semina za ujasiriamali wanaopata, zimewafungua vijana wengi na kutambua umuhimu wa kuunganisha nguvu pamoja, mikopo na urejeshaji, sambamba na mbinu za kufanya biashara na namna ya kupata masoko ya bidhaa wanazoziuza.

       Naye mkurugenzi wa shirika la Vission for Youth, Violet Ayubu, amesema kuwa, shirika lao limejikita katika kuwawezesha vijana kiuchumi kwa kutoa elimu ya uraia, biashara  pamoja na mafunzo ya ujasiriamali na kuwaunganisha na masoko kupitia mitandao, ili kupata masoko kupitia mitandao hiyo, jambo ambalo limewafanya vijana wengi kutulia na kutumia fursa hiyo adhimu.

      "Tunashirikiana na serikali, kuwapa vijana elimu ya biashara na mbinu za kusaka masoko  kupitia kampeni ya Soko Mkononi, tunawaunganisha  vijana kufanya biashara kupitia mitandao, kwa tumia simu zao za mkononi kupata masoko, mitandao ambayo vijana wengi wanapenda, hivyo badala ya kuchati mambo yasiyo ya muhimu, wanatumia kufanya biashara na wengi wanapenda na wananfanikiwa" amesema Violeth  

      Mkurugenzi Violeth ameongeza kuwa, mafunzo hayo, licha ya kuwapa fursa ya kupata elimu ya kupata masoko, yanawajengea uwezo wa kuweka malengo na mikakati ya kukuza mitaji na  kibiashara za kwa kuwa mnyororo wa thamani kupitia biashara zao.

      Mafunzo hayo ya siku moja, yametolewa na halmashauri ya Arusha kwa kushirikiana na shirika la Vision for Youth, yamekutanisha viongozi wa vikindi 11 vya halmashauri za Meru, Arusha na Jiji la Arusha.

  *PICHA ZA MATUKIO YA KIKAO*





Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.