Na Elinipa Lupembe
Viongozi wa makundi ya kijamii tarafa ya Enaboishu, wakiwemo viongozi dini, mila, siasa na wamebainisha kuwa Zoezi la Sensa ya watu na makazi katika maeneo yao litafanyika pasi shaka, kwa kuwa viongi hao wamehamasisha wananchi wao vya kutosha.
Viongozi hao wamemthibishia hayo Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa wilaya na Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ryango, wakati wa kikao kazi cha kuhamsaisha Sensa ya watu na makazi, tarafa ya Enaboishu,,kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano, halmashauri ya Arusha.
Viongozi hao wamweka wazi kuwa, serikali imeweka mikakati mizuri ya kuifanya Sensa ya 2022 kuwa shirikishi kwa kutumia majukwaa mbalimbali kuelimisha na kuhamasisha watanzania umuhimu wa kushiriki Sensa kwa maendeleo ya Taifa.
Aidha wamempongeza mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwa mstari wa mbele kuelezea umuhimu wa sena na umuhimu wa watu kuhesabiwa kwa maendeleo ya Taifa la Tanzania.
Zakayo Mollel, mzee msahuri wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, amethibitisha kuwa Sensa ya mwaka 2022, ni tofauti na sensa nyingine, serikali imetumia majukwaa mengi kuelezea umuhimu wa sensa hii,
"Sisi kama kanisa, kila inapofanyika ibada lazima suala la sensa lihamasishwa, tunakuhakikishia mheshimiwa mkuu wa wilaya, hakuna mtu ambaye hatajesabiwa katika maeneo yetu kwa kuwa kila mtu kwa nafasi yake wa kusikia amesikia na wa kuelewa ameelewa, tuko tayari kuhesabiwa" Amesisitiza Mzee Zakayo Mollel
Naye Shekhe wa Msikiti wa RAHMA Moivo, amesema kuwa, imani ya dini ya kiislamu inaamini sensa ni tukio muhimu kwa maisha ya mwanadamu, kila tunapofanya ibada tunawahamasisha wananch kuhesabiwa, hivyo tunahikia watu watanzania wote watahesabiwa.
Naye Diwani wa kata ya Kimnyaki Mhe. Eliakim Marivei serikali imefanya kazi kubwa sana, kuhakikisha zoezi la sensa ya watu na makazi litafanyika kwa ufasaha na kuongeza kuwa wao kama viongozi wananchi wanaunga mkono juhudi hizo na watasimamia katika maeneo yao kuhakikisha kila mtu aliyelala katika maeneo yao usiku wa kuamkia siku ya sensa anahesabiwa.
Hata hivyo mzee wa mila wa kabila la kimaasai Tarafa ya Enaboishu, Mzee Longishu Mollel, amesema kuwa wananchi wamehamasika na sensa ya mwaka huu, na wao kama viongozi wanaendelea kuhamasisha na kuhahakikisha zoezi hili linafanyika kama yalivyo malengo ya serikali.
Awali Mwenyekiti wa Sensa ya Watu na Makazi wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango, amepata wasaa wa kuwaelezea viongozi hao, umuhimu wa wao kama viongozi kushiriki zoezi zima la Sensa ya watu na makazi.
SHIRIKI SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022
JIANDAE KUHESABIWA 23.08.2022
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.