Viongozi wa vyama vya Siasa wa Jimbo la Arumeru Magharibi Halmashauri ya Wilaya wametakiwa kuhakikisha wanakuwa mabalozi wa Amani na Upendo kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 ,oktoba 2025.
Hayo yamesemwa na Masimamizi wa uchaguzi Jimbo la Arumeru Magharibi Ndugu Stedvant katika kikao cha Viongozi wa vyama vya Siasa kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Ndugu Sdevant Kileo amesema kuwa tangu kuanza kwa Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu kumekuwa na utaratibu wa kukutana na Viongozi wa vyama vya siasa ili kufanya tathimini, kupanga mikakakati ya masuala yanayotarajiwa kufanyika pamoja na kupeana elimu juu ya masuala ya uchaguzi na kuongeza kuwa mwendelezo wa vikao hivi vimesaidia kudumisha hali ya utulivu na Amani pamoja na kuwapa Viongozi wa vyama vya Siasa Ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
”Kwa maudhui ya leo tulikua tunajadili shughuli zilizo mbele yetu ikiwa ni pamoja na kufuata ratiba za kampeni, ufanyikaji wa kampeni, upigaji wa kura, kuhesabu kura pamoja na matokeo ya upigaji kura, na kuhakikisha Amani inakuwepo kwenye uchaguzi mkuu 2025”amesema Kileo
“Kutokana na misingi ambayo tumejiwekea inanipa matumaini mimi kama msimizi wa uchaguzi kuwa tutamaliza zoezi hili la uchaguzi vizuri, kwa Amani na upendo” amesema Kileo
Naye Mwakilishi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Arumeru (Halmashauri ya Wilaya ya Arusha) Ndugu Eric Mkama amesema vyama vya siasa vimeshirikishwa vyema hatua mbalimbali za masuala muhimu ya Uchaguzi na wamejadiliana vyema.
Nae Mwenyekiti wa chama Cha NCCR MAGEUZI Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Wilson Laizer amewaomba Wananchi wote Wa Jimbo la Arumeru Magharibi waliojiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura wajitokeze kwa wingi tarehe 29/10/2025 waweze kuchagua Viongozi watakaowaongoza katika kipindi kingine cha miaka mitano.
Hata hivyo Ndugu Simon Johnson Bayo Kutoka chama Cha Sauti ya Umma amesema kuwa Viongozi wa vyama vya siasa Wilaya ya Arusha wako tayaria kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika na kumalizika kwa Amani na utulivu.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.