Viongozi wawakilishi wa wananchi halmashauri ya Arusha, wameishukuru serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na mheshimiwwa Rais mama Samia Suluhu Hassani kwa kuwajengea vyumba 100 vya madarasa kwa wakati mmoja, katika shule 2 za msingi shikizi na shule 30 za sekondari, kwa ajili ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2022, jambo ambalo wamekiri kuwapunguzi mzigo wa michango wanachi wao.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti, kwenye maeneo yao, maeneo ambayo ujenzi wa vyumba vya madarasa ya mpango wa mapambano dhidi ya UVIKO 19 unaendeleo, viongozi hao hawakusita kushuru na kuipongeza serikali ya awamu ya sita, kwa mrari huo mkubwa wa ujenzi wa vyumba 100 vya madarasa, unaoendelea kutekelezwa kwenye shule za halmashauri ya Arusha kwa wakati mmoja, jambo ambalo wanakiri kuwa halijawahi kutokea katika awamu zilizotangulia.
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Arumeru, Simon Saning'o, amesema kuwa CCM kama wasimamizi wa Ilani, wanashuhudia namna serikali ya awamu ya sita inavyotekeleza Ilani yake kwa vitendo katika maeneo yote Arumeru na nchi nzima, huku ikiwapunguzia wananchi wanyonge, mzigo wa michango ya ujenzi wa madarasa, ambao hufanyika kila mwaka ifikapo mwisho wa mwaka kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza.
"Kujengwa madarasa 100 kwa wakati mmoja ni historia katika halmashauri yetu, haijawahi kutokea, sisi kama wasimamizi wa Ilani tunashuhudia kasi ya ujenzi wa madarasa ambayo, yanaleta matumaini ya kukamilika kwa wakati na tunayomatumaini wanafunzi wote waliochagulia kujiunga na kidato cha kwanza Januari 2022, wataingia wote kwa pamoja darasani tofauti na miaka ya nyuma ambapo wanafunzi walianza form one kwa awamu mbili huku wengine wakisubiri 'second selection', wanafunzi mbao huanza masomo kwa kuchelewa pia" amesema Mwenyekiti Saning'o.
Makamu Mwenyekiti halamshauri ya Arusha, na Diwani wa kata ya Matevesi, Mheshimiwa Freddy Mollel amesema kuwa, serikali ya awamu ya sita, imefanya mabadiliko makubwa katika kuwekeza kwenye miundo mbinu ya shule, jambo ambalo limewapa amani wananchi ambao kipindi hiki huwa wanahangaika kuchangishana na kujenga madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza.
"Wananchi wamefarijika sana na ujenzi wa madarasa unaondelwa katika maeneo mengi, kwa ajili ya kidato cha kwanza, kwa kuwa miezi kama hii, huwa ni nyakati za kushikana mashati na wananchi vijijini ili kujenga madarasa ya Form one, lakini sasa serikali imewapumzisha wananchi na shughuli hizo za ujenzi wa madarasa ya kidato cha kwanza, hata wananchi wetu kwa sasa wana amani na wanaipongeza serikali yao.Amesema Makamu Mwenyekiti huyo.
Naye Diwani wa Kata ya Oloireni Mheshimiwa Erick Semboja, amesema kuwa wananchi wa eneo lake wanaipongeza serikali kwa kuwapunguzia mzigo wa kuchangia ujenzi wa madarasa ya kidato cha kwanza kwa mwaka huu, kwa kuwa kila mwaka huwa kunakuwa na uhitaji wa madarasa kwa mwaka unaofuata.
"Serikali imefanya jambo kubwa sana ambalo, limewapa wananchi kupumzika na michango ya vyumba vya madarasa, kupitia miradi hii wananchi wamejenga imani kunwa kwa serikali yao," amesema Mheshimiwa Erick Semboja.
Julius Mollel mkazi wa Olosiva (57), ameweka wazi kuwa, haijawahi kutokea katika shule yao ya Kiranyi, kujengwa madarasa 13 kwa wakati mmoja na kukamilika ndani ya miezi miwili ama mitatu, mara nyingi huwa tunajenga madarasa mawili ama matatu kwa shida sana, kwa kuchangishana pesa yetu ndogo na wakati mwingine madarasa hayo hushindwa kukamilika kwa ukosefu wa fedha, miezi kama hii hata viongozi wetu wamepumzika pai, maana ndio walikuwa wanahamasisha michango ya ujenzi na kuongeza kuwa mwaka huu watasherehekea sikukuu ya Krismass na mwkaa mpya kwa utulivu.
Halmashauri ya Arusha inajenga jumla ya vyumba 100 vya madarasa, madarasa 96 sekondari na madarasa 4 kwa shule mbili shikizi kwa gharama ya shilingi bilioni 2, fedha za mkopo wenye riba nafuu kutoka Benki ya Dunia, ikiwa ni mradi wa Mpango wa Maendeleo na Ustawi wa Taifa wa Mapambano dhidi ya UVIKO 19.
ARUSHA DC
#KaziInaendelea✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.