Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza kupokea majina ya wagombea watano wa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo kwa Kanda ya Afrika akiwemo pia Prof. Mohamed Janabi ambaye anaiwakilisha Tanzania.
Katika taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya WHO Machi 14, 2025 inaeleza kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Duniani Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amepokea majina ya wagombea watano kutoka nchi wanachama wa WHO Kanda ya Afrika.
Prof Janabi atachuana na Dkt N'da Konan Michel Yao kutoka Côte d'Ivoire, Dkt. Dramé Mohammed Lamine kutoka Guinea, Dkt. Boureima Hama Sambo kutoka Niger pamoja na Prof. Mijiyawa Moustafa kutoka Togo.
WHO itaendesha tena uchaguzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Kanda ya Afrika hivi karibuni kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mteule wa Shirika hilo kilichotokea Novemba 27, 2024.
Fuatilia kurasa zetu kwa habari zaidi za uchaguzi huu.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.