Na. Elinipa Lupembe.
Wafugaji katika halmashauri ya Arusha wamepata neema ya mgao wa za viuatilifu vya kuua dawa ya kuogeshea mifugo ikiwa ni viuatilifu vya kuua vya kuulia wadudu aina ya kupe, mgao huo ni kufuatia mpango wa Serikali ya awamu ya tano wenye lengo la kuhamasisha wafugaji kuogesha mifugo yao, ili kuwa na ufugaji wenye tija.
Wafugaji hao wamepata neema hiyo baada ya Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kutoa jumla ya lita sabini na tano (75) za viuatilifu aina ya 'Paranex' yenye kiini cha 'Alphacypermethtrin yenye uwezo wa kuua wadudu ya kupe kwa ajiki ya wafugaji wa vijiji vitano vya halmashauri ya Arusha.
Akizungumza wakati wa kukabidhi dawa hizo kwa wajumbe wa kamati za uendeshaji majosho za vijiji vinne, zoezi lililofanyika kwenye ofisi za Mifugo makao makuu halmashauri ya Arusha , Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Dkt. Wilson Mahera, amewataka wajumbe hao kwenda kuhamasisha wananchi kuogesha mifugo yao, ili kuzuia vifo vya mifugo vinavyotokana na magonjwa yenezwayo na kupe na mbung'o.
Ameongoza kuwa, tafiti zinaonyesha kuwa, asilimia 72% ya vifo vya mifugo nchini, hutokana na magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa yanayotokana na kupe na ndorobo, na kulisababishia taifa hasara ya takribani bilioni 63 kwa mwaka, huku takribani asilimia 70% ndama wanaozaliwa hufa kila mwaka, hii ni kutokana na wafugaji kukosa mwamko wa kuogesha mifugo yao.
Ili kuzuia vifo hivyo na hasara kubwa inayoligharimu taifa, serikali imeanza kuwawezesha wafugaji kwa kutoa dawa za kuogeshea mifugo ili kuzuia magonjwa yanayoenezwa na kupe pamoja na kuhamasisha wafugaji kuogesha ng'ombe kupitia majosho yaliyo katika maeneo yao.
"Inaonekana wafugaji hawana mwamko wa kuosha mifugo yao, lakini kupitia serikali ya kijiji na ninyi wajumbe wa kamati za uendeshaji majosho, hamasisheni wafugaji na simamieni vizuri zoezi hili ili kila mfugaji aweze kunufaika na huduma hiyo" amesema Mkurugenzi Mahera.
Aidha mkurugenzi Mahera, amewataka wajumbe wa kamati hizo kushirikiana na serikali ya kijiji chini ya usimamizi wa maafisa mifugo wa ngazi zote, kusimamia vema utoaji wa huduma hiyo kwa wafugaji kwa kuhamasisha na kuwahimiza wafugaji kuogesha mifugo yao, pamoja na kusimamia fedha za mapato na matumizi ili mradi huo uwe endelevu.
" Serikali imewapa dawa hizi ni kama mtaji wa kuanzia kutoa huduma ya kuogesha mifugo yenu, mapato yatakayopatikana, yatumike kuendeleza huduma hii kwa wafugaji katika maeneo yenu, shirikianeni na serikali ya kijiji , na zaidi watumieni maafisa mifugo katika maeneo yenu, kupata ushauri wa kitalamu". Amesisitiza Dkt. Mahera.
Naye Daktari wa mifugo, halmashauri ya Arusha, Dkt. Linus Prosper,ametaja bei elekezi iliyotolewa na serikali ya kuendesha huduma hiyo ya kuogesha mifugo, kwa kufafanua kuwa, bei ya ng'ombe mmoja kwa muosho mmoja ni shilingi 50 na shilingi 10 kwa mbuzi na kondoo kwa muosho mmoja.
Hata hivyo serikali imefafanua kuwa gharama hizo zinaweza kubadilika, kulingana na gharama halisi za uendeshaji wa josho katika eneo husika kutegemea maamuzi ya Kamati ya Uendeshaji wa Josho husika.
Aidha Dkt. Linus amezitaja kamati nne za majosho, zilizokabidhiwa dawa kuogesha mifugo ni pamoja na Kamati ya Josho la Engutukoit kata ya Oldonyowas, Oloitushula kata ya Musa, kidali na Engalaoni kata ya Mwandet huku kila Josho likipata lita 10 za dawa.
Hata hivyo wajumbe wa kamati hizo wameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuwakumbuka wafugaji, kwani kwa miaka mingi sasa, serikali ilikua kama imewasahau na kuahidi kwenda kuhamasisha wafugaji kujitokeza kuogesha mifugo yao, kwa gharama nafuu ambazo hapo awali wafugaji wengi walikua wanashindwa kuzimudu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Josho la Oloitushula kata ya Musa, Manase Meoki, licha ya kuishuru serikali kwa kuwakumbuka wafugaji, amesema kuwa uwepo wa dawa hizo, zilizotolewa na serikali utawasaidia kupunguza gharama kubwa walizokuwa wakizitumia pamoja na kuepuka kuuziwa dawa zisizofaa na kuwataka wananchi wenzake kuunga mkona jitihada hizi za serikali.
Halmashauri ya Arusha ina jumla ya majosho 18, majosho nane kati ya hayo ndio yanatoa huduma, majosho matano hayatoi huduma kutokana na uhalisia wa maeneo yalipo tayari kumeshakuwa miji na kuwa katika makazi ya watu hivyo hayatumiki kwa sasa, huku majosho matano yakihitaji ukarabati kutokana na uchakavu uliotokana na kujengwa muda mrefu.
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Dkt. Wilson Mahera akimkabidhi mmoja wa mjumbe wa kamati ya uendeshaji josho (jina halikuweza kupatikana) box lenye lita kumi za dawa.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati za Uendeshaji Majosho, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa dawa za kuogeshea mifugo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.