Na Elinipa Lupembe
Wadau wa Maendeleo halmashauri ya Arusha, kutoka nchini Ujerumani, wameendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mama Samia Suluhu Hassan, katika kuboresha miundombinu ya Afya, lengo likiwa ni kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa jamii, hususani maeneo ya vijijini.
Wadau wa shirika la Help for Maasai Children kwa ufadhili wa marafiki kutoka nchini Ujerumani, wamefanikisha mkakati huo wa serikali kwa kujenga nyumba ya mtumishi wa afya, yenye thamani ya shilingi milioni 30, kwenye zahanati ya Nameloki kijiji cha Losinoni juu Kata ya Oldongowas.
Akizungumza wakati wa kukabidhi nyumba hiyo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha, mwakilishi wa marafiki hao kutoka Ujerumani, Andreas Reinke, amesema kuwa, wamefikia hatua hiyo kwa kuona adha ya upatikanaji wa matibabu kwa wananchi wa Losinoni juu, na kuamua kujenga zahanati na sasa kujenga nyumba ya mtumishi ili wananchi wapate na huduma za dharura hasa nyakati za usiku.
"Tulijenga zahanati, tukaona tujenge nyumba ya mtumishi, ili kuongeza wigo wa upatikanaji huduma za afya kwa wepesi kwa wananchi wa Losinoni, tunaungana na serikali ya Tanzania, kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya unaimarika kwa wananchi wote". Amesema Andreas.
Naye Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, licha ya kuwashukuru wadau hao amekiri kuthamini mchango huo mkubwa kwa wananchi, sambamba na kutekeleza vipaumbele vya serikali ikiwemo kusogeza huduma za afya kwa wanachi kwa lengo la kupunguza vifo vya wanawake na watoto nchini.
Aidha Mkurugenzi Msumi amewataka wananchi wa Losinoni Juu, kuutunza mradi huo pamoja na wahudumu wa afya waliopangiwa kufanya kazi hapo, ili udumu kwa sasa na vizazi vijavyo.
"Wananchi wa Losinoni Juu, mmepata zahanati, serikali imeleta madaktari hapa, hakikisheni mnatunza miundo mbinu na mali zote pamoja na kushirikiana na watumishi hawa, ni ndugu zenu, ni watanzania wenzetu". Amesistiza Mkurugenzi Msumi
Hata hivyo wananchi wa Losinoni juu wamekiri kufurahishwa na uwepo wa zahanati na nyumba ya daktari, kwa kuwa imewarahishishia upatikanaji wa huduma pindi wanapokuwa wagonjwa lakini zaidi kwa kina mama wajawazito na watoto.
Naishiye Lomutiye amebainisha kuwa wajawazito waliteseka sana na kulazimika kujifungulia nyumbani, jambo ambalo ilikuwa ni hatari kwa maisha ya mama na mtoto, kwa sasa hufuma zipo wajawazito watahudumiwa zahanati.
Naye Diwani wa kata ya Oldonyowas, licha ya kuwashukuru marafiki hao, ameipongeza serikali kwa kutoa wahudumu wa afya pamoja na vifaa tiba, vilivyofanikisha utoaji na upatikanaji wa matibabu kwa wananchi.
"Zahanati ilijengwa mwaka 2018, kwa juhudi za serikali mwaka huu tumepata daktari na wauguzi, serikali ya mama Samia inatuthamini sana, wananchi tuendelee kushirikiana na serikali kwa ajili ya maendeleo yetu na Taifa letu". Ameweka wazi Mhe. Kijana.
ARUSHA DC
#KaziIendelee✍✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.