• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wadau wa Mifugo waitaka jamii kuthamini bidhaa za mifugo, zinazotengenezwa na viwanda vya ndani

Posted on: September 12th, 2019

Na. Elinipa Lupembe.

Wadau wa sekta ya mifugo, halmashauri ya Arusha wameitaka jamii, kuachana na dhana potofu ya kudhamini bidhaa za nje ya nchi ni bora kuliko zinazotengenezwa hapa nyumbani, badala yake kuanza kuthamini na kutumia bidhaa zinazotengenezwa na viwanda vya nyumbani, ili kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano na utekelezaji wa uchumi wa viwanda, kuelekea uchumi wa kati.


Wakizungumza katika hafla fupi ya kuwakabidhi vyeti kwa wadau wa mifugo walioshiriki kwenye maonesho ya nane nane mwaka 2019, katika banda la mifugo la halmashauri ya Arusha, wadau hao wamesema kuwa, changamoto kubwa inayokabili wawekezaji wa sekta ya mifugo, ni uelewa duni wa jamii, juu ya mtumizi ya bidhaa zao za ndani na kuthamini zaidi bidhaa kutoka viwanda vya nje ya nchi.


Wamefafanua kuwa, wafugaji wengi wameanza kuamka na kuanza kufuga kibiashara kwa kutumia malighafi za mifugo, kuanzisha viwanda, ikiwemo viwanda vya kuchakata ngozi, kufungasha maziwa na nyama, teknolojia ya gasi itokanayo na kinyesi cha ng'ombe, na kuongeza kuwa changamoto kubwa ni ushindani mkubwa wa bidhaa za nje, unaotokana na dhana potofu ya jamii ya watanzania kutokununua bidha zinazotengenezwa nchini.


Msimamizi wa kiwanda cha Uchakataji Nyama, 'Maasai Exports Butchery', Frenk Mollel, amesema kuwa licha ya kuwa kiwanda hicho, huzalisha bidhaa za nyama zenye ubora wa kimataifa, lakini bado wananchi hawatumii bidhaa hizo kwa wingi, jambo linalosabisha soko la ndani kusuasua.


"Watu kutoka mataifa ya nje wananunua ng'ombe hapa nchini, wanasafirisha nje ya nchi, kule wanatumia mashine kama tunazo tumia sisi, lakini wakiingiza nchini bidhaa hizo, watanzania wananunua bidhaa hizo zaidi na kwa bei ya juu, wakidhani ni bora zaidi, ilihali kiwango cha ubora kinafanana na bidhaa ambazo tunazalisha hapa nchini" amesema Mollel.


Aidha, Mollel ameishauri Serikali na Taasisi zake, kuwa mfano kwa kutumia bidhaa za ndani, ikiwemo nyama inayozalishwa hapa nchini, kwa kufanya hivyo kutawapa hamasa wananchi kutumia bidhaa zinazotengenezwa ndani ya nchi.

Naye mfugaji Leah Sangawe, amesema ng'ombe ni zaidi ya biashara, kwa kuwa  ana uwezo wa kutoa malighafi nyingi tofauti, zinazoweza kuzalisha bidhaa ikiwemo chakula, mavazi, dawa, pamoja na mapambo na kuwashauri wafugaji kutokukatishwa tamaa na changamoto za masoko na kuendelea kuzalisha bidhaaa zenye ubora wa kushindana kwenye soko la kimataifa.


"Ng'ombe hutoa kwato kwaajili ya gundi, mifupa kwa ajili ya mapambo, ngozi kwa ajili ya viatu, maziwa na nyama kwa ajili ya chakula, kinyesi kwa ajili ya Nishati hivyo unapamuuza ng'ombe nje ya nchi unapoteza faida nyingi ambazo zingesaidia kukuza uchumi wa taifa" amesema mfugaji huyo.


Sambamba na hayo, Afisa Mifugo Halmashauri ya Arusha, Charles Ngiloriti, amesema, halmashauri imejipanga kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili wafugaji, ikiwa ni pamoja na kuwatembelea maeneo yao ya kazi, kuwapatia elimu wafugaji ili ku0ngeza thamani ya bidhaa zitokanazo na mifugo.


"Tumekuwa tukiwashirikisha wadau mbalimbali wa mifugo kwenye maonesho, semina na mikutano pamoja na kuwatembelea ili kubaini changamoto pamoja na kuwapatia elimu juu ya ufugaji bora wenye tija katika jamii" amesema Ngiloriti.

Kwa upande wake Daktari wa mifugo Halmashauri ya Arusha, Dkt. Yohana Kiwone amewaambia wadau hao kuwa, Halmashauri ipo kwa ajili ya kuwasaidia wafugaji wote, hivyo wanatakiwa kutumia fursa hiyo, kutatua changamoto zinazowakabili na kufanya uzalishaji bora unaokidhi viwango vya soko la kimataifa.


Awali hafla hiyo, iliyofanyika katika ofisi za Mifigo za Halmashairi hiyo, lengo likiwa ni kuwakutanisha wadau wa mifugo na kuwapa vyeti wadau 8 vya kuwashukuru kwa kushiriki maonyesho ya Nanenane mwaka 2019.


Wadau 8 wa mifugo halmashauri ya Arusha, wakiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Idara ya Mifugo, mara baada ya kukabidhiwa vyeti vya ushiriki wa maonesho ya nanenane.






Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA August 14, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • KUFUATILIA NA USAMIZI WA HAKI ZA MTOTO KATIKA JAMII NI JAMBO MUHIMU

    August 25, 2025
  • RAIS SAMIA AMUAPISHA AMOS MAKALLA KUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA

    August 26, 2025
  • DKT. JAHANNES LEMBULUNG' LUKUMAY ACHUKUWA FOMU YA UGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI

    August 25, 2025
  • KIKAO KAZI CHA WENYEVYITI WA BODI NA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI ZA UMMA (CEOs Forum 2025)

    August 24, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.