WAFANYABIASHARA ARUSHA WAIOMBA SERIKALI KUTUPIA MACHO BAADHI YA SHERIA ZA KODI
Baadhi ya wafanyabiashara wameiomba Serikali kuangalia zaidi utitiri wa sheria za kodi zinazowakandamiza ikiwemo ushuru wa huduma (Service Levy) unaotozwa kwenye Halmashauri mbalimbali nchini ili kuondoa usumbufu kwa wafanyabiashara wanaolipa kodi Serikalini.
Wakitoa maoni yao mbele ha Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi inayoongozwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Balozi Ombeni Sefue wafanyabiashara hao pamoja na wadau mbalimbali wamesisitiza uthamini wa biashara za watanzania hata kwa kuzingatia aina za biashara.
Wafanyabiashara hao akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Wataalam wa Kodi Tanzania Kanda ya Kaskazini, Nicholas Duhia pamoja na Adolf Locken ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji wa Abiria Moose wa Arusha (AKIBOA ) wamesema wao kama Chama waliwasilisha maoni yao kwa Tume hiyo kuhusu sheria za mbalimbali za Kodi inayotozwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) huku wakiomba kodi ya huduma ishuke kutoka asilimia 3 hadi kufika 0.1 kulingana na huduma walizotoa.
"Kila Halmshauri ina malipo yake katika ulipaji wa ushuru wa huduma, hii ni kero lakini wamiliki wa hoteli wameongezewa kodi ya huduma ya takataka wakati magari ya kuzoa taka ni machache hivyo kodi hizi ziwekwe katika dirisha moja ili walipaji walipe kodi kwa kiwango kiridhishi na si kodi kubwa tofauti na ukubwa wa biasgara ya mtu".
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi,Balozi Ombeni Sefue amewasihi wafanyabiashara hao kutoa mawazo yao ili kumsaidia Rais Dkt. Samia Hassan Suluhu kuja na mpango mzuri wa ukusanyaji wa kodi nchini ambao utakuwa ni rafiki kwa pande zote mbili.
"Hakuna mtu yoyote atakayesumbuliwa wakati wa utoaji maoni juu ya ukusanyaji wa mapato hayo lakini Tanzania bado tupo nyuma katika ukusanyaji wa mapato tupo kwenye asilimia 12 lakini sasa tunahitaji kukusanyaji zaidi ya asilimia 15-16 ya mapato kwa nchi za Afrika ikiwemo Tanzania "
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.