Na Elinipa Lupembe
Wafanyabiashara na wananchi wa kata ya Nduruma wameishukuru serikali kwa kutoa eneo la kunzaisha soko la bidhaa za vyakula kijiji cha Samaria, soko ambalo litafanya kazi kila siku na siku moja ya gulio, ukiwa ni mpango wa serikali wa kutenga maeneo rasmi kwa ajili ya kufanyia biashara hususani kwa wafanyabiasha wadogowadogo.
Wananchi hao hususani wafanyabiashara, wamebainisha hayo wakati wa uzinduzi wa soko hilo la Samaria, lililozinduliwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha Mhe. Dkt. Ojung'u Salekwa na kuweka wazi kuwa, walilisubiri soko hilo kwa muda mrefu na sasa serikali ya awamu ya sita imetimiza ndoto zao.
Licha ya kuishukuru serikali, wamethibitisha uwepo wa soko hilo utawawezesha kinamama wa Nduruma kupata sehemu karibu ya kufanyia biashara kutokana na ukweli kuwa, eneo lao halikuwa na soko na kuwalazimu kwenda mbali kufanya biashara na wengine kufanyabiashara pembezoni mwa barabara, na kuipongeza serikali ya mama Samia kupitia serikali yao ya Kijiji kuona umuhimu wa kuwawekea soko ndani ya kata yao.
"Sisi kina mama tulikuwa tunaamka saa nane za usiku ili kuwahi kufika kwenye masoko ya Jiji la Arusha, tulienda soko la Kilombero au Tengeru ili kuleta bidhaa za kuuza kwenye magenge yetu, uwepo wa eneo la soko utatupunguzia kazi ya kwenda masoko ya mbali" Amesema mfanyabiashara Frida Ngolocho
Magdalena Hamadi, amewashukuru viongozi wa kata na kijiji kwa kuanzisha soko rasmi, kwa kuwa walitumia muda mwingi kwenda kufanya biashara mbali kufuata magulio maeneo mengine, sasamwemepata soko la kila siku nyumbani.
Naye Fatuma Mohamed, ambaye ndiye mwanzilishi wa soko hilo amebainisha serikali kuwatendea haki kwa kuweka soko, kuwagawia vizimba na kuweka umeme utakaowawezesha kufanya biashara hadi usiku huku akiwataka viongozi kusimamia vizuri uendeshaji wa soko hilo na kuliboresha ili liwe kubwa zaidi na la kisasa kwa kuwa kuna eneo la kutosha.
"Tunaamini huu ni mwanzo mzuri, tunaiomba serikali kuendelea kuboresha miundo mbinu ya soko hili ili likue na liwe la kisasa zaidi, zaidi tunaomba uongozi wa soko kusimamia vema uendeshaji wa soko hili ili lisife kama ilivyo kwa masoko mengine na kuwasisitiza wafanyabiashara wote kuondoka kwenye maeneo yasiyo rasmi na kuhamia sokoni hapo" Amesema Fatuma
Hata hivyo Diwani wa kata ya Nduruma Mhe. Raymond Mollel, ameweka wazi furaha ya wananchi wa kata hiyo kutokana na kusubiri mchakato wa uanzishaji wa soko hilo uliyochukua miaka mingi, soko ambalo litahudumia kata zaidi ya tatu, kwa kuwa maeneo haya hayana soko karibu.
"Wananchi walilazimika kwenda soko la mjini Kilombero na Tangeru, jambo ambalo kwa sasa wafanyabiashara na wakulima watauza na kunua bidhaa zote hapa, lakini pia wapo kina mama waliofanyia biashara pembezoni mwa barabara, ambayo ilikuwa ni hatari kwa maisha yao, lakini sasa wamepata soko rasmi". Amesisitiza Mhe. Diwani
Awali Soko la Samaria limezinduliwa rasmi na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha Mhe. Dkt. Ojung'u Salekwa kwa kukata utepe na kuwataka wafanyabiashara wote kuondoka kwenye ameneo yasiyo rasmi na kufanyaia biashara zao sokoni, huku akiahidi kuendelwa kuboresha miundombinu ya soko hilo kadri fedha zitakavyopatikana.
ARUSHA DC NI YETU, TUSHIRIKIANE KUIJENGA
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.