Na Elinipa Lupembe.
Wafugaji halmashauri ya Arusha, wakiri kunufaika na teknolojia ya uhimilishaji wa ng'ombe, teknolojia iliyoongeza uzalishaji wa mazao yatokanayo na ng'ombe, mazao yaliyoongeza kipato linalojinasibisha na kilimo biashara.
Wafugaji hao wakiwa wameleta mifugo yao kwenye maonesho ya nanenane Kanda ya Kaskazini, yanayoendelea kwenye viwanja vya Themi - Njiro jijini Arusha, wamekiri teknolojia ya kupandisha ng'ombe kupita chupa kulemeta mapinduzi makubwa katika uzalishaji na ongezeko la mazao ya mifugo.
Abraham Abraham,mfugaji kutoka kitongoji cha Olturumet, amekiri matumizi ya teknolojia ya uhimilishaji imeleta mapinduzi makubwa kwa wafuga, kwa kuwapatia ng'ombe bora, wanaokua haraka huku wakizalisha maziwa na nyama nyingi zaidi.
Amefafanua kuwa wafugaji kwa sasa, wanajivunia teknolojia hiyo, na kumuelezea ng'ombe wake wa miezi 20 mwenye jina la Spika, ambaye ana uzito wa kilo 60 tayari ana mimba ya miezi 6, mwenye uwezo wa kutoa lita 30 mpaka 35 za maziwa kwa siku, maziwa ambayo yakiuzwa yanaleta kiiasi cha shilingi elfu 49 kwa siku.
"Ngombe huyu ni mtamba ambaye amepatikana kwa kutumia teknolojia ya Uhimilishaji, ni mchanganyiko wa mbegu za fresian na asian, na amesajiliwa kwa namba 0001642, mwenye uwezo wa kutoa maziwa lita 30 -35 kwa siku, huku maziwa hayo yakiingiza takribani shilingi milioni 17.6 kwa mwaka" Amebainisha mfugaji Abraham Abraham
Alfayo Mollel, amebainisha kuwa teknolojia ya uhimilishaji imewapa matumaini wafugaji, na kuongeza kuwa kwa sasa mradi wa ufagaji ng'ombe, unajiendesha wenyewe kupitia maziwa yake na kuleta faida kubwa tofauti na ufugaji wa zamani ambapo ng'ombe alitoa lita 3 za maziwa kwa siku.
"Teknolojia hii imeleta matumaini kwetu wa wafugaji, upatikanaji wa maziwa mengi umeniwezesha kuanzisha kiwanda cha kusindika maziwa pamoja na matumizi ya gesi ya samadi 'bio gas' Amefafanua Alfayo
Naye Daktari wa Mifugo halmashauri yaArusha Dkt. Yohana Kiwone, amethibitisha ubora wa teknolojia ya uhimilishaji na upatikanaji wa ngombe bora wenye kuleta faaida kubwa kwa wafugaji sasa.
Dkt. Kiwone amewasisitiza wafugaji kubadilika na kufanya kilimo biashara kwa kutumia teknolojia za kisasa huku wakifuta maelekezo ya watalamu kwa ajili ya kupata mazao bora.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.