• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WAHITIMU JKT OLJORO WATAKIWA KUWA MFANO WA KUIGWA KWENYE JAMII.

Posted on: September 12th, 2023

Na Elinipa Lupembe

Vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa Oparesheni ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa, wametakiwa kutumia ujuzi na maarifa waliyopata kipindi cha mafunzo kwa kulitumikia Taifa na kuwa mfano wa kuigwa na vijana wote ndani ya jamii.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda, wakati akifunga mafunzo ya miezi mitatu ya Oparesheni miaka 60 ya JKT, KJ833 Oljoro, kwa kuwataka vijana hao, kwenda kutumia ujuzi na maarifa waliyoyapata kulitumikia taifa la Tanzanzia pamoja na kuwa mfano wa kuigwa na vijana wenzao ambao hawajapata fursa ya kupitia mafunzo haya ndani ya jamii.

Mhe. Emmanuela licha ya kuwapongeza vijana hao, amewasisitiza kwenda kutekeleza kwa vitendo yale yote waliyojifunza ili kutimiza uahalisi wa mafunzo kwa kuonesha utofauti  kati yao na vijana wasioshiriki mafunzo haya kwa kuonesha umahiri na uzalendo kwa nchi yao

"Leo vijana mmeonesha umahiri mkubwa uliotupa taswira ya jinsi wakufunzi wamewafundisha ukakamavu, uzalendo, utiifu na umahiri, mmeitendea haki heshima ya  Amiri Jeshi Mkuu,  mmeonyesha uaminifu kwake kama JKT na jeshi kwa ujumla, hivyo katumieni maarifa haya kulitumikia Taifa na sio vinginevyo" Amesisitiza Mkuu wa wilaya

Ameongeza kuwa, umefika wakati wa kuanza maisha ya kujitegemea, mmepita kipindi cha uangalizi wa wazazi na walimu, sasa mko tayari kujisimamia, tumieni vizuri uhuru wenu kwa kutekeleza majukumu binafsi na yale mtakayopangiwa kwa kuzingatia kanunia taratibu,  sheria za nchi kwa kuheshimu mila na desturi za jamii sambamba  na kuepuka tabia hatarishi ikiwemo matumizi yasiyo sahihi ya mitandao,  yanaweza kuwaingiza kwenye migogoro ya kisheria.

Hata hivyo wahitimu hao, wameishukuru serikali kwa programu hiyo muhimu kwa vijana wa kitanzania na kukiri kujengewa uwezo mkubwa wa kujitambua na kujithamini,  kujiamini na kujitegemea, uzalendo, utiifu, uhodari na umahiri, utakaowawezesha kulitumikia Taifa lao na watanzania kwa ujumla.

Naye Mhitimu 'service girl' Anna Tumainiel Minja, amesema kuwa mafunzo hayo yamewatoa kwenye ulimwengu wa giza na kuwaleta kwenye mwanga ambao utakuwa dira ya maisha yao katika kulitumikaia Taifa la Tanzania

"Wengi tulikuja tukiwa na hofu kumbwa, kumbe mambo ni tofauti, JKT inatoa mafunzo ambayo yanatujengea uwezo mkubwa wa kuwa vijana wenye kulitumikia Taifa kwa uzalendo na sio ubinafsi" Amesema Anna

"JKT imetujenga kiafya na kiakili, tumejifunza kuwa wachapakazi, kuwa wavumilivu katika nyanja zote za maisha, kuwa watii kwa wakubwa na wadogo, kuwa wazalendo kwa nchi yetu, kuwa hodari na mahiri katika kufanya kazi zetu binafsi na zile tutakazopangiwa, ni jambo zuri sana kwa vijana wa kitanzania, tunaahidi kutumikia kiapo tulichokula leo kwa nchi yetu" Eliud Long'idare

Salam Loi Mzazi wa Idd Haruna, ameishukuru Mungu na serikali na kuweka wazi kuwa mwanzo walikuwa na hofu kubwa lakini ameshuhudia mabadiliko makubwa ya kitabia kwa mtoto wake,  amezidisha nidhamu, na amekiri kutamani kijana wake kuendelea kubaki jeshini kuliko kubaki mtaani

Awali kwa mamlaka aliyopewa Mkuu wa wilaya ya Arumeru amefunga mafunzonhayo nprasmi huku jumla ya vijana 3,319 wa kundi la lazima wamehitimu mafunzo ya oparesheni ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa katika kikosi cha JKT Oljoro.


#KaziInaendelea✍✍


PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA KUFUNGA MAFUNZO




Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • DKT. PASCAL KATIKA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

    June 19, 2025
  • WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

    June 18, 2025
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI

    June 17, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.