• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WAJUMBE WA BARAZA LA MADIWANI ARUSHA DC WAMALIZA MUDA WAO KWA MAFANIKIO MAKUBWA YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Posted on: June 11th, 2020

Na. Elinipa Lupembe.

     Wajumbea wa Baraza la Madiwani halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru, wameridhishwa na utekelezaji wa shughuli za maendeleo zilizofanyika kwa kipindi cha miaka mitano cha uongozi wao, kipindi cha kuanzia mwaka 2015 mpaka 2020.

     Wamesema hayo wakati wa Mkutano maalum wa Baraza la Madiwani wa kuvunja baraza hilo, baada ya madiwani hao, kulitumikia baraza hilo kisheria kwa muda wa miaka mitano ya kikatiba na hatimaye kufikia ukomo wa kulivunja rasmi, mkutano uliofanyika, kwenye ukumbi wa mikutano, halmashauri ya Arusha,

       Madiwani hao wametoa shukurani na pongezi zao za dhati, kwa halmashauri ya Arusha na Serikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na mheshimiwa Rais Dkt.John Pombe Magufuli, kwa kufafanua kuwa, Baraza limefanikiwa kufanyakazi kwa mafanikio makubwa, katika kuleta maendeleo ya kijamii kisekta, kuanzia ngazi ya kitongoji, kijiji, mkata na halmashauri kwa ujumla kutokana na uwezeshwaji mkubwa kutoka serikalini kupitia watalamu wa halmashauri.

    Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, Baraka Simoni, amehitimisha kuwa, kwa kipindi chote cha miaka mitano, baraza hilo limefanyakazi ya kuwatumikia wananchi kwa mafanikio makubwa katika utekelezaji wa shughuli za  maendeleo katika sekta zote, kufuatia taarifa ya miaka mitano, iliyowasilishwa kwenye Baraza hilo.

     "Ninawishukuru serikali na watalamu, Baraza hili, limemaliza muda wake kwa mafanikio makubwa ukilinganisha na awamu zilizopita, kutokana na support kubwa iliyotoka serikali kuu chini ya uongozi wa jemedari Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kuwezesha utekelezaji wa miradi mikubwa katika seka za elimu, afya, maji, umeme na barabara"

     Akihitimisha Baraza hilo kwa niabavya Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Afisa Tawala wilaya, mwalimu James Mchembe, licha kupongeza mafanikio hayo yaliyofanikiwa kwa ushirikiano mkubwa wa serikali, watalamu na madiwanj hao, amewatakia madiwani hao kila la heri katika mpambano mwingine wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka 2020, na kuwasihii kugombea kwenye chama imara kitakachowawesha kurudi madarakani.

     Akisoma taarifa ya utendaji kazi wa shughuli za halmashauri ya Arusha, taarifa iliyoweka wazi mafanikio hayo, kwa kipindi cha miaka mitano cha kuanzia mwaka 2015, Afisa Mipango, halmashauri ya Arusha, Anastazia Tutuba, amesema kuwa, katika kipindi cha miaka mitano, halmashauri imefanikiwa kutekeleza majuku yake halmashauri, imefanikiwa kuongeza mali zake na kushughulikia madeni kutoka mali za shilingi milioni 60.4 mwaka 2015 na kufikia mali zenye thamani ya shilingi milioni 71.5.

      Imeelezwa kuwa hamashauri imeendelea kuimarisha mikakati ya ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mashine, kutoka makusanyo ya shilingi bilion 2.4 mpaka kufikia bilioni 3.5, pamoja na mafanikio hayo, halmashauri imeweza kufanya matumizi yanayozingatia sheria, kanuni na taratibu za matumizi ya fedha za Umma, na kufanikiwa kupata hati safi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa miaka 7 mfululizo mpaka sasa.

    Aidha, halmashauri imefanikiwa kuboresha sekta ya elimu kwa kuboresha miundombinu ya shule, na kujenga jumla ya vyumba vya madasa 140, sekondari madarasa 87 na  madarasa 53  shule za Msingi, nyumba za walimu 55, huku kukiwa na ongezeko la ufaulu kutoka asilimia 80 mpaka 100%.

      Halmashauri imepokea kiasi cha shilingi bilioni 9.12,fedha za elimu bila malipo, ikiwa shilingi bilioni 3.1  kwa shule za msingi na shilingi bilion 6 kwa shule za sekondari zikiwa ni fedha za uendeshaji shule, fedha za chakula, ruzuku ya fidia ya ada pamoja na posho za madaraka.

     Kupitia programu Lipa kutokana na Matokeo (EP4R), Halmashauri imefanikiwa kuoboresha miundombinu ya shule za sekondari na mringi kwa kukakarabati, kujenga na kumalizia maboms ya vyumba vya madarasa, maabara za masomo ya Sayansi, mabweni, mabwalo ya chakula, maktaba, mabweni pamoja na ununuzi wa samani.

Kupitia mkakati wz serikali wa kuboresha shule zake kongwe, halmashauri pia ilipata shilingi milioni 927 kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzani (TEA) za kukarabati shule ya sekondari Ilboru,pamoja na shilingi milioni 70 za ujenzi wa bweni la wasichana shule ya sekondari Einoth.

     Kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani, Halmashauri imetumia kiasi cha shilingi bilioni 1.3 kwa kutoa mikopo kwa vikundi 314 vya wanawake, vijana na walemavu huku jumla ya wanawake 2,446, vijana 502 na walemavu 20 wamenufaika na mikopo hiyo kulinganisha na awamu zilizopita.

      Mafanikio makubwa yamejitokeza katika uboreshaji na utoaji huduma za Afya, upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi kupitia  vituo 57 vya kutolea huduma za afya huku hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, ukiimarika kutoa asilimi 83.5 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 93.4.

     Aidha vituo vya kutolea huduma za afya vimeongezeka kutoka 47 mpaka kufikia 57, huku hali ya miundombinu ya vituo hivyo, ikifanyiwa ukarabati, jumla ya vituo viwili vya afya vimepanuliwa na kuwa na hadhi ya nyota 5, kituo cha Afya Nduruma kimetumia kiasi shilingi milioni 500 na Mbuyuni shilingi milioni 400, fedha kutoka Serikali Kuu pamoja na ujenzi wa zahanati ya Musa uliogharimu shilingi milioni 200 fedha P4R.

   Kufuatia sera ya uanzishwaji wa kulekea uchumi wa kati ifikapo 2025, halmashauri haikuwa nyuma, imefaviwandanikiwa kuratibu na kuboresha mazingira bora kwa wafanyabiashara wakubwa na wajasiriamali wadogo,kwa kuwajengea uwezo wa uwanzisha viwanda, na hadi sasa halmashauri kuna jumla ya viwanda 377, viwanda vidogo, 350, viwanda vya kati 26 na kiwanda kikubwa 1.

       Hata hivyo viwanda hivyo, vimejikita uzalishaji wa bidhaa za samani, usindikaji wa vyakula, vinywaji na mvinyo, kuchana mbao, kutengeneza matofali, vifungashio,batiki, viwatilifu, vyandarua,vipodozi, kuchakata ngozi na uchomeleaji na uungaji vyuma.

Awali mafanikio hayo, yametokana na juhudi kubwa za serikali ya awamu ya tano, waheshimiwa madiwani waliomaliza muda wao, watalamu wa halmashauri ya Arusha, wadau wa maendeleo pamoja na wananchi wote wa halmashauri ya Arusha.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, Mheshimiwa Baraka Simon akizungumza na Madiwani wa halmashauri hiyo, wakati wa Mkutano Maalum wa Baraza la madiwani la kuvunja baraza hilo baada ya kutumikia kwa mika mitano tangu mwaka 2015 ya kikatiba.


Katibu Tawala wilaya ya Arumeru, mwalimu James Mchembe, akitangaza kuvunjwa kwa Baraza la Madiwani, wakati wa Mkutano Maalum wa Baraza la madiwani la kuvunja baraza hilo, baada ya kutumikia kwa mika mitano tangu mwaka 2015 ya kikatiba.


Afisa Mipango halmashauri ya Arusha, Anastazia Tutuba, akisoma taarifa ya  mafanikio ya utekelezaji wa shughuli za Maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano 2015-2020, wakati wa Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani wa kuvunja baraza hilo, baada ya kutumikia kwa miaka mitano ya kikatiba.








Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.