Wajumbe wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wiaya ya Arusha wamekaa kikao cha robo ya pili ya mwaka cha utoaji wa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa Kata zote 27 na kupokea taarifa za kila Kata kabla ya Kikao cha Baraza la Madiwani cha tarehe 13/01/0225.
Wajumbe wa kikao hicho wameendelea kuipongeza Serikali inayogonzwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ndani ya Halmashauri hiyo ikiwemo miradi ya Afya,Elimu,Miundombinu,Maji,pamoja na umeme.
Sambamba na pongezi hizo wajumbe wa Baraza hilo la Madiwani Halmashauri ya Arusha pia wametoa rai yao kwa ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Arusha kuendelea kuweka juhudi za ziada kutekeleza miradi ya maendeleo katika Halmashauri hiyo kwa kushirikiana na watalaamu kutoka Taasisi zingine za umma kama vile AUWSA,RUWASA,TARURA,TANESCO na nyinginezo Ili kufanikisha utatuzi wa changamoto kwa wananchi
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.