WAKALA WA BARABARA VIJIJINI TARURA WATAKIWA KUTATUA KERO YA MIUNDO MBINU NA KUUNGANISHA VITONGOJI KWA VIVUKO.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha ndg Thomas Loy Sabaya amewataka Viongozi wa Wakala wa barabara Vijijini (TARURA) kuhakikisha kuwa wanatatua changamoto ya miundombinu iliyoharibiwa na mvua za masika kufanya haraka kuunganisha vivuko vilivyokuwa vikiunganisha Vitongoji kwa Vitongoji ili wananchi waendelee kupata mawasiliano kama ilivyokuwa awali.
Ndugu Sabaya ameyasema hayo alipokuwa kwenye mwendelezo wa ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kata ya MOIVO alipokuwa akipokea na kusikiliza kero za wananchi wa kata hiyo.
Akiwa kata hiyo,Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Arusha amewakumbusha viongozi wa Chama na Serikali kuwa majukumu yao ya msingi ni pamoja kusikiliza na kutatua kero za wananchi wanaowangoza kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama likiwemo jeshi la Polisi.
Aidha,ndugu Sabaya amewataka wananchi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha Kata ya Moivo wanapambana kupiga vita dawa za kulevya ikiwemo bangi na kuwa ajenda huvyo inapaswa kuwa ya kudumu kwanini athari za matumizi ya dawa hizo kwa vijana ni hatari kwa nguvu kazi ya Taifa.
Sambamba na hilo,Ndugu Sabaya aliitaka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA), TANESCO NA TARURA kufika katika Kata ya Olmotony kutatua changamoto ya huduma ya Maji , Umeme na Miundombinu ya barabara inayowakabili wananchi wa Kata hiyo.
Naye Mwenyekiti wa Halmashaurii ya Wilaya ya Arusha Dkt.Ojung'u Salekwa aliyembatana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa katika Ziara hiyo alimshukuru Mwenyekiti wa CCM Mkoa kuwa sehemu ya ziara hiyo kwani kuna mengi amejifunza na kuahidi kusimamia Miradi yote ya Maendeleo kwa Ubora na hasa kuangalia thamani halisi ya vifaa vinavyonunuliwa.
Pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha amewataka wananchi kuhakikisha wanalinda na kutunza Miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekezwa kwenye maeneo yao ,ili iweze Kudumu na kusaidia Jamii Kama ilivyokusudiwa
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.