• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WAKUFUNZI WA SENSA MKOA WA ARUSHA WATAKIWA KUFANYAKAZI KWA WELEDI

Posted on: July 27th, 2022

Na Elinipa Lupembe.

Wakufunzi wa Sensa ya Watu na Makazi mkoa wa Arusha, wametakiwa kuwa waadilifu, wazalendo na kutumia weledi wa hali ya juu katika kufanikisha zoezi la Sensa, inayotarajiwa kufanyika nchini tarehe 23, August 2022.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongela, wakati akifunga mafunzo ya siku 21 kwa wakufunzi wa Sensa ngazi ya mkoa, mafunzo yaliyofanyika, kwenye ukumbi wa mikutano chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) .

Mkuu huyo wa mkoa amewataka wakufunzi hao, ambao watakwenda kuwafundisha makarani wa maudhui ya Sensa ngazi ya Halmashauri, kwenda kufanya kazi hiyo kwa uadilifu, uzalendo na weledi hasa kwa kuzingatia umuhimu na madhumuni ya Sensa ya Watu na Makazi kwa wananchi na serikali kwa ujumla.

"Kwa kutambua umuhimu wa Sensa ya watu na makazi, serikali imewaamini na kuwapa mafunzo ya muda mrefu ili muweze kufanyakazi hiyo kwa weledi kwa kuzingatia kanuni na taratibu za kazi hiyo, hivyo ni vema mkatambua mnakwenda kufanya kazi nyeti kwa manufaa ya Taifa letu la Tanzania" Amesisitiza Mkuu huyo wa mkoa.

Hata hivyo Mhe. Mongela, amesisitiza kuwa endapo mtakwenda kuwafundisha makarani wa Sensa kwa weledi, mtaiwezesha serikali kupanga mipango yake ya maendeleo kwa kuzingatia idadi ya watu ambao zoezi la kufanikisha hili liko mikononi mwenu, niwatake mkafanye kazi hii kwa kujiamini kama serikali ilivyowaamini.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha, Steven Zelote, amewasihi wakufunzi hao, kufanya kazi hiyo vema na kuhakikisha mkoa wa Arusha unakuwa kinara wa Sensa ya Watu na Makazi nchini.

Naye mwanasemina na Afisa Elimu kata ya Olmotonyi, halmashauri ya Arusha, mwalimu Denis Machallo, amesema kuwa, wanatambua umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi kwa serikali yao, hivyo kupitia mafunzo hayo, wameahidi kwenda kufanya kazi hiyo kwa weledi hasa kwa kuzingatia mustakabali wa Taifa la Tanzania na kwa kuweka uzalendo mbele na kuhakikisha wanahawilisha maarifa waliyoyapata kwa makarani wa maudui ngazi za halmashauri kama ilivyo malengo ya serikali.

"Tumepewa mafunzo kwa siku 21, wawezeshaji wamefanya kazi yao vema, hivyo tunakwenda kutekeleza jukumu hili la kitaifa, kwa kuzingatia maslahi mapana ya taifa letu la Tanzania na sio vinginevyo ili kuhakikisha zoezi la Sensa linafanikiwa kwa zaidi ya asilimia 100 katika mkoa wetu wa Arusha". Amesisitiza Mwalimu Machallo.

Awali mkufunzi mkuu wa mafunzo hayo, Mdoka Omari, ameweka wazi kuwa, jumla ya wakufunzi 399 kutoka halmashauri zote 7 za mkoa wa Arusha, wamepatiwa mafunzo ya Sensa ya Watu na Makazi ambao watakwenda kuwafundisha makarani wa sensa katika halmashauri zao.


*SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022*

*JIANDAE KUHESABIWA*✍



Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongela, wakati akifunga mafunzo ya wakufunzi wa Sensa ya Watu na Makazi ngazi ya Mkoa, mafunzo yaliyofanyika, kwenye ukumbi wa mikutano chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) .





Wakufunzi wa Sensa ya watu na Makazi ngazi ya Mkoa wa Arusha, wakimskiliza mkuu wa mkoa wa Arusha, mhe. John Mongela wakati akifunga mafunzo hayo, kwenye ukumbi wa mikutano chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) .





Mkufunzi mkuu wa mafunzo mkoa wa Arusha, Mdoka Omari akisoma taarifa ya hali halisi ya mafunzo hayo wakati wa kuhitimisha mafuzo hayo, yaliyofanyika, kwenye ukumbi wa mikutano chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) .


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, mkoa wa Arusha Steven Zelothe (wa kwanza kulia) akiwa kwenye hafla ya kufunga mafunzo kwa wakufunzi wa Sensa ngazi ya mkoa, kwenye ukumbi wa mikutano chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) .







Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.