• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WAKULIMA WA MBOGAMBOGA SAMBASHA WAPEWA SOMO LA KILIMO BORA CHENYE TIJA

Posted on: September 10th, 2022

Na Elinipa Lupembe.


Kufuatia mkakati wa Serikali wa kufikia Ajenda 10/30 ya Kilimo Biashara, halmashauri ya Arusha, inaendelea tekeleza mpango huo kwa vitendo kwa kuwapati vikundi vya wakulima wanaojishughulisha na kilimo cha mbogamboga kata ya Sambasha, mafunzo ya kilimo bora cha kisasa na chenye tija.

Akizunguza na mwandishi wa habari hizi, Afisa Kilimo kata ya Sambasha Anna Lorry, amethibitisha kuwa jumla ya wakulima 155 wa kata hiyo, wamepatiwa mafunzo kupitia shamba darasa lililopo eneo la Tengeru, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kufanya kilimo cha kisasa, kitakachowawezesha kufanya biashara kupitia mazao wanayolima.

Afisa Kilimo huyo amebainisha kuwa, kwa sasa  wakulima wa eneo hilo wameanza kubadilika na kulima kisasa kwa kutumia eneo dogo na kuzalisha mazao mengi, na kuachana na kilimo cha mazoea,  ambacho kiliwapatia faida ndogo.

"Wakulima wamefundishwa kutumia eneo dogo kupata mazao mengi, uchaguzi wa mbegu bora, matumizi ya mbolea na dawa sahihi za kuulia wadudu pamoja na kufanya tafiti za masoko kabla ya kuamua kulima zao husika kulingana na msimu" . Amefafanua Afisa Kilimo huyo.

Hata hivyo wakulima hao licha ya kuishukuru Serikali kwa kuwa na mikakati imara kwao, wamekiri mafunzo hayo kuwapa ujuzi na maarifa mapya ikiwa ni pamoja na mbinu sahihi za kuwawezesha kufanya kilimo biashara, jambo ambalo wamekiri hapo awali waliliona  kama ni ndoto.

Wameongeza kuwa, mafunzo hayo yamewatoa kwenye kilimo cha cha mazoea na kuwaaminisha kwamba kilimo biashara kinawezekana kupitia maeneo yao, wanayoyatumia kulima kwa miaka yote, ambayo walitumia nguvu na gharama kubwa na kupata faida kidogo.

"Awali sikuelewa Kilimo biashara nilidhani ni propaganda tuu, kupitia mafunzo mbalimbali tunayopatiwa na serikali kwa kushirikiana na wadau wa kilimo, ninatumia ujuzi nilioupata, ninaamini kilimo biashara inawezekana na tunaweza kufikia Ajenda 10/30 kwa vitendo" . Amesema Mosses Njivai mkulima kijiji cha Shibolo.

Njivai amethibitisha kuwa, awali hatukuwa tunafanya tafiti za masoko kabla ya kulima, jambo ambalo lilisababisha kuuza mazao kwa bei ya hasara kutokana na mafuriko ya mazao wakati wa mavuno, program ya Anzia Sokoni Malizia Shambani kwa kipato zaidi inatufanya kuwa watafiti wa masoko kabla ya kulima.

Awali Halmashauri ya Arusha kwa kushirikiana na wadau wa kilimo, wanaendelea kutoa elimu na mbinu za kilimo bora kwa wakulima, lengo likiwa ni kuongeza pato la mkulima na kufikia Agenda 10/30 ya Kilimo Biashara.


ARUSHA DC TUPO KAZINI

AJENDA 10/30 TUNATEKELZA

KAZI INAENDELEA ...✍✍















Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.