• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WAKUU WA KAYA TOENI USHIRIKIANO KWA MAKARANI WA SENSA SIKU YA SENSA..

Posted on: August 21st, 2022

Na Elinipa Lupembe ARUSHA DC

Wananchi halmashauri ya Arusha hususani wakuu wa kaya, wametakiwa kutoa ushirikiano kwa makarani wa Sensa, wakati wote wa zoezi la Sensa ya watu na makazi kwa kutoa taarifa zote sahihi zinazohitajika kwenye dodoso la Sensa.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Arumeru, wakati wa kuhitimisha Matembezi ya Hiari ya kuhamasisha Sensa ya watu na makazi, kwenye stendi ya  Ngaramtoni, Katibu Tawala wa  wilaya hiyo, Mwl. James Nchembe, amewataka wananchi wa halmashauri hiyo hususani wakuu wa kaya, kutoa ushirikiano kwa makarani wa Sensa watakapofika kwenye kaya zao kukusanya taarifa za Sensa.

Amesema kuwa kwa kufanya hivyo, kutawezesha makarani hao kupata taarifa sahihi zitakazowesha kupata takwimu sahihi zinazohitajika na Serikali kwa ajili ya kupanga mipango yake sahihi kwa maendeleo ya watanzania wote..

"Utoaji na upatikanaji wa Takwimu sahihi utawezesha serikali na wadau wengine kupanga mipango ya maendeleo ya watu wake katika sekta ya elimu, afya, hali ya ajira, miundombinu ya barabara, maji safi na nishati, mipango ambayo itawezesha upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi". Amesistiza Katibu Tawala huyo.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, ameeleza kuwa lengo la matembezi hayo ya hiari ni kuhamasisha wanachi wa halmashauri hiyo, kushiriki zoezi la Sensa ya watu na makazi na kuhakikisha kila mtu amehesabiwa siku hiyo ya tarehe 23.08.2022 na kuwasisitiza wakuu wa kaya kuhakikisha kila mtu aliyelala kwenye kaya yake siku hiyo amehesabiwa.

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi, Mhe. Noah Lembris,  ameeleza kuwa suala la Sensa ya watu na makazi ni jambo la muhimu sana kwa  wananchi wa Jimbo hilo, na kuwasihi wananchi wote kuhakikisha wamehesabiwa ili serikali iweze kuoanga mipango ya maendeleo katika jimbo hilo.

Monica Lema mkazi wa Oloirien, amewataka wananchi wote kuhakikisha wamehesabiwa siku hiyo ya Sensa ya Watu na makazi, jambo litakalosadia kuweza kupata maendeleo kwani serikali itajua idadi sahihi ya Watu ambayo itawezesha serikali kupata takwimu sahihi kwa ajili ya kupanga kwa usahihi utoaji wa huduma za msingi kutokana na takwimu za idadi ya watu.

Katika matembezi hayo, halmashauri kwa kushirikiana na wadau wa afya, wameweza kutoa huduma za kupima  afya bure  kwa wananchi wote walifika kwenye shughuli hiyo katika eneo la Ngaramtoni  ikiwemo ugonjwa, homa ya ini, saratani ya shingo ya kizazi, UKIMWI, kisukari na shinikizo la damu.


HAKIKISHA UMEHESABIWA 23.08.2022









Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.