Walengwa wa TASAF walio kwenye mpango wa Kunusuru kaya masikini kijiji cha Naurei, wakipatiwa mafunzo ya kuunda vikundi vya kuweka akiba, kuwekeza na kukopeshana.
Mafunzo hayo ni utekelezaji wa programu ya TASAF ya kuwajengea uwezo walengwa hao, kuwa na tabia chanya ya kujiwekea akiba, zaidi kuwekeza fedha za kukopeshana kwa ajili ya kuanzisha miradi ya uzalishaji.
Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Arusha Grace Makema, amesema kuwa, vikundi hivyo vitaendelea kusimamiwa na watalamu wa fani za mtambuka za Maendeleo ya Jamii, kilimo, mifugo, biashara na ujasiriamali ili kuviwezesha kubuni miradi midogo midogo ya uzalishaji.
" Uanzishwaji wa vikundi hivyo, unalenga zaidi kuongeza pato la familia kupitia miradi ya uzalishaji watakayokuwa wanaifanya kwa usimamizi wa watalamu kutoka halmashauri". Amefafanua Mratibu Grace
Hata hivyo walengwa hao, wamepongeza juhudi hizo za serikali za kuendelea kubuni mbinu za kuinua pato la kaya zilizo kwenye mpango wa kunusuru Umasikini.
Juliana Daniel, amesema kuwa, serikali imekuwa ikiwajali sana walengwa licha ya kuwapa fedha, bado imeendelea kuwa na mipango endelevu ya kuhakikisha walengwa hao wanaimarika kiuchumi
"ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
#kaziinaendelea✍✍✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.