• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WALIMU SEKONDARI ARUSHA DC WATAKIWA KUACHA KUFUNDISHA KWA MAZOEA BADALA YAKE KUTUMIA MBINU ZA KISASA

Posted on: April 14th, 2021

Na. Elinipa Lupembe.

Walimu wa shule za sekondari halmashauri ya Arusha wametakiwa kuacha kufundisha kwa mazoe badala yake, kuongeza kasi, juhudi na maarifa katika ufundishaji kwa kutumia kutumia mbinu za kisasa,  ili kuendsna na wakati lengo likiwa kupandisha kiwango cha taaluma kwa wanafunzi pamoja na kupandisha hali ya ufaulu kwa wanafunzi kwa shule za halamshauri hiyo.

Rai hiyo imetolewa na kamati ya Mitihani ya halmshauri hiyo, wakati wa  kikao kazi cha tathmini ya matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne ya mwaka 2020, kilichowakutanisha wakuu wa shule, walimu wa taaluma wa shule zote za sekondari pamaja na waratibu wa Elimu wa kata zote za halmashauri ya Arusha, kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa shule ya msingi ya Green Acress.

Kamati hiyo ya mitihani imetoa rai hiyo mara baada ya baadhi ya wakuu wa shule na walimu wa taaluma waliofanya vizuri kudilishana uzoefu, kwa kuelezea mbinu wanazotumia kufundisha, zinazosababisha matokeo mazuri katika shule zao.

Mwenyekiti wa kamati ya mthihani halmashauri ya Arusha na mkurugenzi mtendaji, Saad Mtambule, amewataka wakuu wa shule na waratibu elimu kata, kufuatilia utekelezaji wa shughuli za ufundishaji na nidhamu kwa walimu na wanafunzi, kwa kuhakikisha kila mmoja anatekeleza wajibu na majukumu yake ya kila siku,mjambo ambalo litapandisha taaluma na kuongeza ufaulu.

"Mbinu hizi zilizotolewa na walimu walifanya vizuri, si mbinu mpya basi ni kiasi cha walimu kuacha kufundisha kwa mazoea na kuzifanya mbinu hizo kwenda na wakati wa sasa, kiuhalisia  changamoto za shule zetu zinaoendana, niwatake walimu walimu kutumia changamoto hizi kuwa fursa na kuamua kujiwekea malengo kwa kujitoa, kufundisha, kupima na kutahmini matokeo ya utendaji, kufuatia malengo mliyojiwekea" amesisitiza Mkurugenzi huyo

Aidha walimu hao wa shule zilizopata matokeo mazuri, wameweka wazi kuwa, shule zao zinazimejikita katika kufanyakazi kama timu, kwa kuwaandaa wanafunzi kitaaluma na kinidhamu, huku walimu wakihakikisha wanafundisha mada zote na kukamilisha kwa wakati na kutoa mazoezi, majaribio na mitihani ya mara kwa mara kwa kuwafuatilia pamoja na kufanya tathmini ya matokeo ya upimaji huo.

Mkuu wa shule ya sekondari Ilboru mwalimu Denis Otieno,amefafanua kuwa licha ya kuwa shule ya sekondari Ilboru inapokea wanafunzi wenye ufaulu wa juu, bado shule inafanya juhudi za ziada za ufundishaji ili kuhakikisha wanafunzi hao, wanafanya vizuri katika masomo yao, tangu wanapoingia shuleni hapo mpaka kufanya mitihani yao ya mwisho.

"Tumepanga safu ya ufundishaji kimasomo kupitia kila idara, safu ambayo inahakikisha masomo ya idara husika yanafundishwa ipasavyoa 'effectively', huku wanafunzi wakipewa mazoezi, majaribio na mitihani ya kutosha, pamoja na kuwa na idara ya ukaguzi na upimaji inayofuatiliaji na kukagua utekelezaji wa kazi zote za kitaaluma na nidhamu kwa walimu na wanafunzi" amefafanua mkuu huyo wa shule

Hata hivyo wakuu wa shule ambao shule zao hazikufanya vizuri, wameeleza kuridhishwa na kikao kazi hicho, kilichowapa mwanga na uzoefu kutoka kwa shule nyingine, uzoefu ambao wameahidi kuufanyia kazi, lengo likiwa ni kupandisha kiwango cha taaluma na kuongeza ufaulu katika shule zao.

Awali katika kiako kazi hicho, uongozi wa halmashauri ya Arusha, umewapongeza, wajumbe wa kamati ya mitihani,  Idara ya elimu sekondari,  Waratibu Elimu kata, Wakuu wa shule, walimu wa taaluma pamoja na walimu wote kwa ujumla, kwa kuwezesha halmashauri hiyo kuendelea kupata matokeao mazuri kwa mitihani ya taifa ya kidato cha pili, cha nne na cha sita mwaka hadi mwaka, , na kuwataka kujipanga kutokomeza alama sifuri.

Kikao kazi hicho cha tahmini, kiliambatana na utoaji wa zawadi za pongezi kwa Wakuu wa shule 3 zilizofanya vizuri katika halmashauri hiyo, pamoja na walimu waliofaulisha masomo yao kwa alama A, B na C, kwa kupewa vyeti na pesa taslimu huku shule zilizofanya vibaya zikipewa vyeti vyenye rangi nyekundu kuashiria hatari (tafsiri isiyo rasmi).

Kwa mwaka wa masomo 2020, jumla ya wanafunzi 4,881 walifanya mtihani wa kidato cha nne kutoka shule 49 za halmashauri hiyo,na ufaulu wa jumla ukiwa ni  asilimia 92.65 kufuatia malengo ya halamshauri ya kufikia asilimia 90,  huku ubora wa ufaulu ukifikia asilimia 41.73 kwa wanafunzi waliopata daraja la I mpaka la III.



Mwenyekiti wa kamati ya Mitihani na Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Saad Mtambule, akizungumza na wakuu wa shule na walimu wa taaluma shule za sekondari za halamshauri hiyo, watumishi idara ya Elimu pamoja na Waratibu wa Elimu kata zote, wakati kikao kazi cha tahmini ya matokeo ya mtihani wa kidato cha IV mwaka 2020, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa shule ya msingi Green Acres.


Mwenyekiti wa Hashauri ya Arusha, mheshimiwa Ojung'u Salekwa, akizungumza na wakuu wa shule na walimu wa taaluma shule za sekondari za halamshauri hiyo, watumishi idara ya Elimu pamoja na Waratibu wa Elimu kata zote, wakati kikao kazi cha tahmini ya matokeo ya mtihani wa kidato cha IV mwaka 2020, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa shule ya msingi Green Acres.

Afisa Elimu sekondari, halmashauri ya Arusha, Mwalimu Menard Lupenza, akiwakaribisha wajumbe wa kikao cha tahmini ya matokeo ya mtihani wa kidato cha IV mwaka 2020 kwa kueleza  lengo la kikao kazi cha hicho cha tahmini ya matokeo ya mtihani wa kidato cha IV mwaka 2020.


Mkuu wa shule ya sekondari Ilboru, mwalimu Denis Otieno, akielezea mbinu bora wanazotumia kupata matokeo mazuri kwa watahiwa wa kidato cha nne katika shule yake.


Wakuu wa shule, walimu wa taaluma shule za sekondari halmashauri ya Arusha, wakifuatia mijadala mbalimbali wakati wa kikao kazi cha tathmini ya matokeo ya kidato cha nne mwaka 2020 kwa shule zote za halmashauri ya Arusha.


Wakuu wa shule, walimu wa taaluma shule za sekondari halmashauri ya Arusha, wakifuatia mijadala mbalimbali wakati wa kikao kazi cha tathmini ya matokeo ya kidato cha nne mwaka 2020 kwa shule zote za halmashauri ya Arusha.




Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA August 14, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MKURUGENZI MTENDAJI WA HALASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA BW. SELEMAN MSUMI AWASHONEA SARE MADEREVA WA HALMASHAURI HIYO

    October 02, 2025
  • WIZARA YA KILIMO KUPITIA MAMLAKA YA UDHIBITI WA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO (COPRA) YAZINDUA RASMI MSIMU WA UNUNUZI WA ZAO LA PARACHICHI KWA MWAKA 2025/2026

    September 27, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA ARUMERU MWINYI AHMED MWINYI AHITIMISHA MAFUNZO YA JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT)

    September 21, 2025
  • MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA AWAASA WANANCHI KUJENGA UTAMADUNI WA USAFI

    September 21, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.