• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WALIMU WAJENGEWA UWEZO MATUMIZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO

Posted on: September 12th, 2022

Na Elinipa Lupembe

Walimu wakuu shule za msingi, halmashauri ya Arusha wamejengewa uwezo wa namna bora ya matumizi ya fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika shule zao.

Walimu hao wamepata fursa hiyo, wakati wa kikao kazi maalum, chenye lengo la kuhakikisha kila mwalimu anafahamu Sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya matumizi ya fedha za Umma, katika utekelezaji wa miradi, kikao kilichofanyika kwenye ukumbi mdogo wa mikutano wa halmashauri hiyo.

Mkuu wa Idara ya Mipango, halmashauri ya Arusha, Anna Urio, amefafanua kuwa lengo kikao kazi hicho ni kujenga uelewa wa pamoja juu ya taratibu za matumizi  ya fedha za Umma, zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika halmashauri.

"Kila mwenye dhamana ya kutekeleza mradi anatakiwa kufahamu kiasi cha fedha kilichoingia, muda wa utekelezaji na ukamilishaji wa mradi, kuzingatia 'value for money' ubora wa mradi unaoendana na thamani ya fedha, pamoja na ushirikishwaji wa jamii katika utekelezaji wa miradi". Amefafanua Afisa Mipango Anna.

Serikali imeweka taratibu za matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo hivyo, ni wajibu wa kila mwenye dhamana ya kusimamia mradi unaotekelezwa na fedha za Umma kuufuata lengo likiwa kuwa na uwazi na ukweli katika kusukuma gurudumu la maendeleo.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi, halmashauri ya Arusha, Hilda Mwangamila, amezitaja hatua muhimu za kufuata wakati wa matumizi ya fedha za miradi ni pamoja na kufahamu thamani ya mradi, namna ya kupata wakandarasi na wazabuni kupitia ushindani kwa kuzingatia bei halisi ya soko, pamoja na uteuzi wa kamati za usimamizi wa mradi.

Aidha Mweka Hazina, halmasahuri ya Arusha, David Rubibira, amesisitiza kuwa, wakati wa utekelezajiwa mradi ni lazima kuhakikisha mkandarasi analipa kodi zote za serikali, pamoja na asilimia 5 ya gharama ya mkataba 'retaintion', fedha ambayo endapo itatokea tatizo lolote pesa hiyo itatumika, pesa ambayo itazuia mpaka kazi itakapokamilika.

Hata hivyo walimu hao, wameupongeza uongozi wa halmashauri, kwa kikao kazi hicho ambacho wamekiri kina manufaa kwao, kutokana na ukweli kwamba, utekelezaji wa miradi ya maendeleo unahitaji usimamizi imara wenye kufuata taratibu za matumizi ya fedha za Umma.

Mwalimu mkuu shule yaMsingi Ilboru, Mwl. Philomena Mbilinyi amekiri kunufaika na kikao kazi hicho kwa kuwa yeye ni mara yake ya kwanza kusimamia mradi, maelekezo waliyopewa yatamuwezesha kusimamia mradi huo kwa usahihi kwa kuzingatia malengo ya serikali na kwa manufaa ya Umma.

"Hii ni mara yangu ya kwanza kuanza kusimamia mradi, na shule yangu inamepatiwa shilingi milioni za kutekeleza miradi miwili, ujenzi wa darasa na uzio wa shule, kupitia kikao kazi hiki, kitanisaidia kufanya taratibu sahaii za utekelzaji wa miradi yote, ikamilikekwa wakati ikiwa na ubora unaoendan9a na thamani ya fedha" .Amesisitiza Mwl. Philomina.

Halmashauri ya Arusha, imepokea kiasi cha shilingi milioni 589.5 kutoka Serikali Kuu, kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya miundo mbinu ya shule za msingi na sekondari, miradi ambayo itatekelezwa kwa kipindi cha miezi mitatu.














Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.