Na. Elinipa Lupembe.
Halmashauri ya Arusha, imeadhimisha kilele cha siku ya Mazingira Duniani mwaka 2022, kwa kuwataka wakazi wa halmashauri hiyo, kutunza mazingira kwa kupanda miti huku walimu wakisistizwa kuhakikisha kila mwanafunzi anaotesha mti shuleni kwakwe na kuutunza mpaka atakapohitimu masomo yake shuleni hapo.
Rai hiyo imetolewa na mgeni rasmi, kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Arumeru, Katibu Tawala wa willaya hiyo, Mwalimu James Mchembe, wakati akizungumza na wakazi wa halmashauri ya Arusha, kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani, maadhimisho yaliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Nduruma, kata ya Nduruma.
Katibu Tawala huyo ameweka wazi kuwa, inafahamika umuhimu wa kutunza mazingira ni pamoja na kupanda miti, na kuwataka walimu kuwasimamia wanafunzi katika shule zao, kwa kuhakisha kila mwanafunzi anapanda mti mmoja na kuutunza mpaka atakapohitimu masomo yake katika shule husika.
"Kama kila mwanafunzi atapanda mti, tutakuwa na miti minginkatika maeneo yetu, lakini zaidi miti ya matunda itawapatia watoto lishe itakayotokana na mazao ya miti hiyo ya matunda watakayoipanda, niwasihi walimu kila mwanafunzi awe na mti wake na ndio alama atakayoicha shuleni" amesistiza Mwl. Mchembe.
Hata hivyo Katibu Tawala huyo, alimnukuu mwandishi mmoja wa kitabu, aliyesema moja kati ya mambo matatu muhimu yanayoweza kumfanya binadamu akaacha kumbukumbu katika historia ya maisha yake duniani ni kupanda mti, na kusisitiza kuwa kila mtu anawajibu wa kuacha kumbukumbu kwenye mazingira yake kwa kupanda mti.
Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha amesema kuwa, kila mwananchi analo jukumu la kutunza mazingira, kutokana na ukweli kwamba, uharibifu wa mazingira umesababisha madhara makubwa duniani, ikiwemo uhaba wa mvua na ongezeko la joto, madhara ambayo tayari yanaonekana dhahiri katika maisha yetu.
Aidha amewata watalamu wa mazingira kuendelea kuelimisha na kuhamasisha jamii, hususani wanafunzi, ili wafahamu umuhimu wa kutunza mazingira, zaidi wawe na nasaba na mazingira yao, jambo ambalo litaleta matokeo chanya.
Awali Mkuu wa Idara ya Mazingira halmashauri ya Arusha, Zuraika Mkundya, licha ya juhudi kubwa inayofanywa na idara hiyo kwa kushirikiana na wadau, bado kuna changamoto ya ushitiki mdogo wa baadhi ya viongozi unaosababisha migogoro ya kimazingira, uchafuzi na uharibifu wahifadhi za mazingira.Katika kuadhimisha kilele cha wiki ya mazingira dunia, yenye kauli mbiu, Tanzania ni Moja tuu, Tunza Mazingira, halmashauri imepanda jumla ya miti mia tisa, katika shule za kata ya Nduruma
ARUSHA DC
#KaziInaendelea✍✍
PICHA ZA MATUKI WAKATI WA KILEKE CHA SIKU YA MAZINGIRA
Katibu Tawala, wilaya ya Arumeru, Mwl. James Mchembe, akipanda mti wa maembe kwenye eneo la shule ya msingi Nduruma, wakati wa maadhimisho ya Kilele cha siku ya Maaingira Duniani 2022.
Mwenyekiti halmashauri ya Arusha, Mhe. Ojung'u Salekwa, akipanda mti wa machungwa kwenye eneo la shule ya msingi Nduruma, wakati wa maadhimisho ya Kilele cha siku ya Maaingira Duniani 2022.
Kaimu Mkurugenzi na Mwanasheria Halmashauri ya Arusha, Wakili Msomi, Monica Mwailolo mti wa maembe kwenye eneo la shule ya msingi Nduruma, wakati wa maadhimisho ya Kilele cha siku ya Maaingira Duniani 2022.
Wanafunzi wa shule ya msingi Nduruma wakipanda miti kwenye eneo la shule yao, wakati wa maadhimisho ya Kilele cha siku ya Maaingira Duniani 2022.
Mwalimu mkuu shule ya msingi Nduruma, Mwl. Conjesta Kimaro akipanda mti w kwenye eneo la shule ya msingi Nduruma, wakati wa maadhimisho ya Kilele cha siku ya Maaingira Duniani 2022.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.