WALIOCHANGIA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI KUMI WAPONGEZWA
Madiwani wapongeza na kumshukuru ndugu Bathlomeo Ngeseyan na rafiki zake kwa uzalendo wao wa kuchangia fedha kiasi cha zaidi ya Shilingi milioni kumi kwaajili ya kutatua changamoto ya maji na ukaratabati wa majengo ya vyumba vya maabara katika shule ya Sekondari Losinoni iliyoko Halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru. Pongezi na shukrani hizo imetolewa leo Tarehe 05 Novemba 2024 katika Baraza Kuu la Madiwani lililofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.