• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WAMILIKI WA ARDHI KIJIJI CHA KISERIANI WAPAGAWA NA URASIMISHAJI.

Posted on: February 25th, 2021

Na. Elinipa Lupembe.

Wananchi wanaomiliki ardhi katika kijiji cha Kiseriani kata ya Mlangarini, halmashauri ya Arusha, wamejitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa ya urasimishaji unaofanyika katika maeneo yao, wakati wa utekelezaji wa mradi wa urasimishaji Ardhi katika kijiji hicho, mradi unaotekelezwa na halmashauri ya Arusha kupitia walaamu wake wa ndani.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, alipotembelea eneo la Kiserian, wamiliki hao wa ardhi, wamekiri kuchangamkia fursa hiyo, waliyodai imekuja wakati muafaka na kupongeza juhudi za halmashauri hiyo, kwa kutekeleza mradi wa urasimishaji ardhi katika kijiji cha Kiseriani na vitongoji vyake, zoezi lililoshirikisha wananchi wote katika hatua zote.

Katibu wa Kamati ya Urasimishaji Kitongoji cha Losirwai, Lomayan Maiko Mollel, ameweka wazi kuwa, wananchi wa Kiseriani, wameupokea mradi wa urasimishaji kwa matumaini makubwa,  ndio maana wamejitokeza kwa wingi, kurasimisha maeneo yao waliyokuwa wanayamiliki kihalali lakini bila ya kuwa na vibali halali vinavyoatambulika kisheria, kutokana  na maeneo hayo kutokuwa yamepimwa wala kuwa na ramani ya mipango miji, pamoja na gharama kubwa za urasimihsaji zilizokuwa zinatozwa hapo awali.

"Kiukweli wananchi wa Kiseriani, wamefuhishwa na kuridhishwa na urasimishaji wa maeneo yao, kutokana na kufanyika kwa gharama nafuu, tangu zoezi linaze katika kitongoji changu tuu, cha Losirwai zaidi ya watu 150 wameshalipia na wengine wanaendelea kulipa, na baada ya kulipia tuu,  watalamu wanaweka  bicon bila kuchelewa, kupitia zoezi hilo wananchi wamepata imani kubwa na serikali yao, naweza sema tumepagawa" amesisitiza Katibu huyo.

Hata hivyo wananchi hao, wamekiri kupata muamko mkubwa, kutokana na elimu waliyopewa na watalamu pamoja na  gharama nafuu za urasimishaji, kwa kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakimilki maeneo yao bila vibali maalumu vya serikali kutokana na kushindwa kumudu gharama zilizokuwa zinatozwa, na kuongeza kwamba  zoezi hilo limekuja wakati muafaka, wakiamaini litasaidia kuondoa migogoro ya ardhi iliyokuwa inajitokeza kutokana na udanganyifu uliokuwa unafanywa na watu wasio waaminifu na kwa kuchukulia kigezo cha uelewa mdogo wa watu wengi.

Rick Nkya mmiliki wa eneo kitongoji cha Losirwai na Longiva, amesema kuwa, ushirikishwaji uliotolewa na watalamu wa Ardhi, umefanya wananchi kuwa na uelewa mkubwa juu ya umuhimu wa mipango miji, na kuongeza kuwa kuna athari kubwa za kuishi kwenye maeneo yasiyopangwa, maeneo ambayo hakuna miundombinu ya kueleweka huku wananchi wakijenga nyumba zao bila mpangilio, lakini huku Kiseriani kila mwenye kiwanja amekubali kutoa mita tano mpaka 6 kwa ajili ya barabara za ndani ya mitaa.

"Binafsi ninaishi Sakina, wakati nikinunua kiwanja hakukuwa kumepimwa wala kupangwa, kila mtu amejenga anavyojisikia,  jambo ambalo limeasababisha, ukosefu wa miundo mbinu ya barabara, mpaka sasa kila mtu ana kinjia cha kufika nyumbani kwake tu na baadhi ya watu hawana kabisha njia, jambo linalosababisha migogoro mingi miongoni mwa majirani, hata hivyo gharama zake ni nafuu"amefafanua Nkya.

Naye Mratibu wa Urasimishaji, halmashauri ya Arusha na Afisa Mipango  Miji, Faiz Mnaro, amesema kuwa, tayari wananchi wamepata elimu ya Urasimishaji, na wamejitokeza kufanya utambuzi  na upimaji wa maeneo yao, pamoja na kukubaliana uwepo wa miundombinu ya barabara katika maeneo yao, na kuongeza kuwa kutokana na upimaji kila mtaa utakuwa na barabara za kuanzia  Mita 5 - 6, huku barabara za kuunganisha vijiji na miji zitakuwa na upana wa kuanzia Mita 8  - 15.

Aidha Mnaro, ameelezea faida za urasimishaji ni pamoja na kuondoa migogoro ya ardhi, kumiliki ardhi kisheria ukiwa na kumbukubu halali na hatimaye kupata hati, ardhi inapanda thamani ikiwa imepangwa na kupimwa, inainua maisha ya watu kwa kuweza kupata mikopo na pia kama dhamana kwa lolote, zaidi shughuli za maendeleo zinafanyika kwa kasi katika maeneo yaliyopimwa, na kufafanua kuwa urasimishaji ni zoezi kutambua maeneo na mipaka, inafuata kupima, na kupata hati miliki.

Halmashauri ya Arusha inaendelea na zoezi la urasimishaji katika kijiji cha Kiseriani katika vitongoji vya Kiseriani, Longiva na Losurwai, ambapo jumla ya viwanja 3,051 vimetambuliwa na vinatarajiwa kupimwa na kurasimishwa kwa kuandaa ramani ya Mipango Miji pamoja na wamiliki hao kupatiwa hati miliki.










Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.