Na Elinipa Lupembe
Jumla ya Wanafunzi 10,674, wavulana 5,779 na wasichana 4,894, halmashauri ya Arusha wanategemea kufanya mtihani kwa Taifa wa kuhitimu darasa la saba unafanyika tarehe 13 na 14 Septemba 2023 kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).
Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa Kamati ya Mitihani halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amebainisha kuwa mtihani huo wa Taifa unajumuisha shule za msingi 143, ikiwa shule 95 ni za seikali na shule 48 ni za binafsi.
Ameeleza kuwa, tayari maandalizi yote yamefanyika kwa mujibu wa taratibu za Mitihani ya Taifa huku wanafunzi na walimu wasimamizi wameshapewa mafunzo ya usimamizi wa mtihani huo.
Msumi amewataka wasimamizi wa mitihani, kuzingatia Kanuni, Sheria na Taratibu wakati wote wa mitihani na kutokujiingiza kwenye aina yoyote ya vitendo vya udanganyifu kwa kuwa, lengo la mitihani hiyo ni kuwapima wanafunzi kulingana na kile walichojifunza kwa miaka yote saba.
"Ninawasositiza watalamu wote wanaohusika na usimamizi wa mitihani, kujiepusha na vitendo vilivyo kinyume kinyume na maadili ya mitihani, na kuhakikisha mitihani inafanyika kwa uaminifu kwa kuzingatia haki za watoto hao ili waweze kufikia ndoto zao na sio kuwaingiza kwenye matatizo yasiyo ya lazima, serikali imewaamini na kuwakabidhi jukumu hilo kubwa kwa Taifa, hakikisheni mnalitekeleza kwa weledi, uaminifu na uadilifu". Amesisitiza Mkurugenzi Msumi
Awali Mkuu wa Idara ya Elimu Awali na Msingi, halmashauri ya Arusha, Mwl. Salvatory Alute, amefafanua kuwa kati ya watahiniwa hao 10, 673 wavulana ni 5,779 na wasichana ni 4,894.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Idara, amesema kuwa walimu wamewaandaa wanafunzi vema kisaikolojia, kiakili na kimwili, kwa kuwajengea uwezo wa kujiamini wakati wote wa mitihani kwa kuwa mtihani huo ni sawa na mitihani mingine ambayo huifanya mara kwa mara kwa kipindi chote cha miaka saba wawapo shuleni.
Uongozi wa halmashauri ya Arusha unawatakia wanafunzi wote kila la kheri katika mitihani yao na kuwa watulivu ili waweze kufaulu na kufikia ndoto zao.
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.