• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WANAFUNZI WALIO KATIKA SHULE ZA KUTWA ZA UMMA NA BINAFSI WAPATE CHAKULA

Posted on: September 3rd, 2024

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa @ortamisemi Mohamed Mchengerwa amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kote nchini kuhakikisha wanafunzi walio katika shule zote za kutwa za umma na binafsi wanapata chakula bila kujali ni wa madarasa ya mitihani ama lah na kamati za shule ziimarishe usimamizi wa chakula kinachotolewa na wazazi kwa ajili ya mpango wa chakula shuleni.


Pia amewataka kuendelea kusimamia kikamilifu fedha zote zinazopangwa za kutekeleza afua za lishe na kusimamia ubora wa taarifa ili taarifa zinazoletwa katika ngazi za juu ziwe zinaakisi uhalisia katika jamii.


Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa mkutano wa tathimini ya mkataba wa lishe na kutambulisha mpango wa taifa wa uwekezaji katika afya ya mama na matoto nchini uliofanyika kwenye ukumbi wa Jiji - Dodoma kuanzia tar 30 - 31 Agosti,2024.


Pia amesema kwa Shule za bweni zinazopata fedha kwaajili ya chakula ni vyema kuhakikisha chakula kinachutumika mashuleni ni kile kilichoongezewa virutubishi na ameelekeza wazabuni wa chakula shuleni kupeleka chumvi yenye madini joto,unga na mafuta ambayo hayameongezwa virutubishi.


Pia amewataka kusimamia ubora wa huduma za Afya na kutokomeza kabisa malalamiko ya wananchi dhidi ya ubora wa huduma na vitendo vingine vinavyochonganisa Serikali na wananchi na kukamilisha ujenzi na ukarabati wa miradi ya maendeleo katika sekta ya Afya.


Kwa upande wa Waziri wa Afya, Jenista Mhagama amewaomba wakuu wa mikoa na wilaya kujipanga kutoa elimu kuhusu bima ya afya kwa wote na kuhakikisha wanafanya kampeni ya mtu ni afya ili kuondoa magonjwa ya mlipuko hasa magonjwa ya kipindupindu.


“Kwa uwekezaji ambao umefanywa na serikali katika utoaji wa huduma za afya tukishindwa kukiondoa kipindupindi tutakuwa hatujitendei haki sisi watanzania.”


Aidha, Jenista amesema katika kuhakikisha mikataba ya lishe inatekelezwa kwa tija, Wizara yake itahakikisha inakamilisha kwa haraka Sera ya Taifa ya Chakula na Lishe na kushirikiana na sekta binafasi ili chakula cha watoto shuleni kiongezewe virutubisho.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.