• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wanafunzi watakiwa kushiriki michezo inayoendeshwa kwenye shule zao

Posted on: May 29th, 2019

Na. Elinipa Lupembe.

Wanafunzi wenye vipaji vya michezo, wametakiwa  kushiriki  michezo, inayoendeshwa kwenye shule zao,  kwa kuwa ni sehemu ya taaluma itakayowawezesha kupata fursa ya kupata ajira hapo baadaye, pamoja na kukuza taaluma na kuimarisha afya zao.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi  Mtendaji, Halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera, wakati akifungua mashindano ya  michezo kwa shule za msingi - UMITASHUMTA, ngazi ya Halmashauri, ufunguzi uliofayika kwenye viwanja, vya shule ya Sekondari ya Ilboru, kwa lengo la kupata timu itakayoshiriki mashindano hayo ngazi ya mkoa.

Mkurugenzi huyo, amefafanua kuwa, licha ya kuwa michezo ni afya na inakuza taaluma, michezo pia ni fursa kubwa inayomuwezesha mchezaji, kupata ajira yenye maslahi mazuri ndani na nje ya nchi, na kuwasisitiza wanafunzi wenye vipaji kushiriki kwenye michezo inayoendeshwa shuleni kwa sasa.

Dkt. Mahera, ameongeza kuwa Serikali, imeona umuhimu wa michezo na kuamua, kurudisha michezo na mashindano kuanzia ngazi ya shule za msingi, ili kukuza vipaji vya wachezaji tangu wakiwa na umri mdogo, pamoja na kuwaanda wanafunzi wenye vipaji kupata ajira kwenye sekta ya michezo hapo baadaye.

"Michezo kwa sasa ni sehemu ya ajira tofauti na zamani, wapo wachezaji wanalipwa pesa nyingi, pengine kuliko wafanyakazi wengine, na imesaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa ajira kwa vijana katika taifa letu, hivyo Serikali ikaona ni vema michezo irudishwe shuleni" amesema Dkt Mahera

Aidha amewasihi wachezaji watakaochaguliwa, kufanya juhudi na kuwa na nidhamu wawapo kambini, ili kuiwakilisha halmashauri  vizuri kwenye mashindano ngazi ya Mkoa na baadaye ngazi ya taifa.

Naye Afisa elimu Msingi, Mwalimu,  Hossein Mghewa, amewataka wazazi, kuwapa watoto nafasi ya kuonyesha vipaji vyao, kwani michezo huburudisha, hujenga nidhamu, afya, umoja na hatimaye kuongeza kipato kwa familia na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake, mwanafunzi Zahara Khaleed wa shule ya Msingi Ngaramtoni, anayecheza mpira wa miguu, amethibitisha kuwa, michezo inawajengea uwezo wa kujiamini, nidhamu, huimarisha afya pamoja na kukuza mahusiano mazuri kati yao, na shule moja na nyingine,  na kuwataka wazazi kuwaruhusu watoto wao, kushiriki michezo wawapo shuleni.

"Michezo inatusaidia kielimu, tunafundishwa nidhamu na kuimarisha  Afya zetu, zaidi inatusaidia kutujengea mahusiano mazuri kati ya shule yetu na shule zingine na kutufanya tuishi kwa pamoja" amesema Mwanasoka huyo.

Awali, Mratibu wa Michezo ya UMITASHUMTA, Halmashauri ya Arusha, Mwalimu, Khalifa Kiyembe, amesema kuwa, mashindano ya UMITASHUMTA yalianzia ngazi ya kata kwa kushindanisha shule kwa shule na mpaka sasa jumla ya wachezaji 400 wamefanikiwa kufikia,  ngazi ya halmashauri, kupitia wachezaji hao na timu zao, watachaguliwa wachezaji bora 100, kuiwakilisha   halmashauri kwenye ngazi ya mkoa.

Mwalimu Kiyembe amebainisha kuwa, mashindano ya UMITASHUMTA  mwaka 2019, yenye kauli mbiu ya 'Michezo na Sanaa kwa Elimu bora na Ajira',  yanashirikisha  mpira wa  miguu kwa wavulana na wasichana, mpira wa pete, mpira wa wavu, mpira wa mikono, riadha, mpira kwa wenye uono hafifu, pamoja na waimbaji.













Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.