Wajumbe wa ALAT Mkoa wa Arusha, wamewapongeza wananchi wa halmashauri ya Arusha kwa jitihada zao kubwa za kuchangia miradi ya maendeleo katika vijiji vyao.
Wajumbe hao wametoa pongezi hizo, walipotembelea miradi 8 ya sekta ya elimi, afya na maji yenye thamani ya takribani shilingi bilioni 9.6 huku asiliamia kubwa ya miradi hiyo, ikichangiwa na nguvu za wananchi.
Katika miradi iliyotembelewa jumla ya shule tatu zimejengwa kwa nguvu za wananchi, shule hizo ni pamoja na shule ya sekondari Losikito, kata ya Mwandeti ambayo imesajiliwa na imeshaanza kufanyakazi, shule ya sekondari Likamba kata ya Musa, inayojengwa na wananchi wa kijiji cha Musa, na shule ya sekondari ya Oldonyowas.
Licha ya pongezi hizo, Wajumbe hao wa ALAT mkoa wa Arusha, wamewataka wananchi wote wa mkoa wa Arusha, kuiga mfano huo wa kuchangia maendeleo yao na kuondokana na dhana ya kusubiri serikali kuwaletea maendeleo katika maeneo yao.
Naye Mwenyekiti wa ALAT mkoa wa Arusha
Mheshimiwa Sabore Molloimer, amesema kuwa ipo haja ya wananchi sasa kutambua kuwa maendeleo yao, yanaletwa na wananchi wenyewe na si kusuburi serikali au misaada kutoka nchi za nje.
"Wananchi hawa, wameonesha wazi kuwa maendeleo yanawezekana kwa kufanya maamuzi na sio kuwa na utajiri mkubwa" amesema Mheshimuwa Mwenyekiti huyo.
Aidha miradi mingine iliyotembelewa ni pamoja na mradi wa maji wa jiji vitano unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Uingereza -DFID,unaotekelezwa na shirika la Water, ujenzi wa Ofisi ya Uthibiti Ubora wa shule, mradi uliotekeleza na Wizara ya Elimu.
Mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa uliofadhiliwa na ubalozi wa Japani nchini Tanzania, ujenzi Jengo la Mama na Mtoto, hospitali ya Olturumet kupitia Mapato ya Ndani pamoja na ujenzi wa maktaba na ukarabati wa Bwalo, shule ya sekondari Mwandeti kupitia miradi ya EP4R.
Wajumbe wa ALAT mkoa wa Arusha, wakikagua jengo la Ofisi ya Uthibiti Ubora wa Shule,halmashauri ya Arusha.
Wajumbe wa ALAT mkoa wa Arusha, wakikagua mitambo ya kuchujia maji kwenye Mradi wa maji wa Vijiji Vitano.
Mitambo ya kuchuja maji, mradi wa maji wa vijiji vitano.
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera akitoa maelekezo ya ramani ya mradi wa maji wa vijiji vitano.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.