Na. Elinipa Lupembe.
Wananchi halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru, wamewatakiwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii, kwa kufuata sheria za nchi pamoja na kumuunga mkono juhudi za mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, katika kupambana na rushwa, dawa za kulevya na kupinga adui ujinga, kwa maendeleo ya Taifa letu na kuelekea uchumi wa kati, ifikapo 2025.
Rai hiyo imetolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2019, ndugu Mzee Mkongea Ali, wakati wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo kwenye halmashauri hiyo, na kuwasisitiza wananchi kuwa, Serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii ikiwemo, huduma za afya, elimu, maji na miundombinu ya barabara, hivyo wananchi wanapaswa kuuunga mkono juhudi hizo kwa kufanyakazi kwa bidii.
Amewasihi wananchi wote, kuhakikisha wanatunza mazingira na vyanzo vya maji, ili waweze kuendelea kupata maji safi na salama, na kuongeza kuwa, kwa kuwa maji ni haki ya kila mtu, hivyo ni wajibu wa na kila mwananchi kutunza vyanzo hivyo vya maji.
"Suala hili la kutunza vyanzo vya maji ni letu sote, niwasihi wananchi wenzangu kuacha, kuchunga mifugo yetu katika hifadhi za misitu yenye vyanzo vya maji, pamoja na kuacha kufanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji" amesisitiza Mzee Mkongea Ali.
Aidha amewataka wananchi wote, kuwa tayari kushiriki uchaguzi unaokuja wa Serikali za Mitaa, na kuwahimiza muda utakapofika, kwenda kujioredhesha kwenye orodha ya wapiga kura, na kuwahamasisha wanawake na vijana kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi zinagombaniwa.
Zaidi Kiongozi huyo, amewataka wananchi, kujitokeza kusikiliza sera za wagombea hao na kufanya maamuzi sahihi ya kuchagua kiongozi, ambaye ataweza kuongoza vyema na kuwaletea maendeleo, na kuachana na vitendo vya rushwa.
Awali katika halmashauri ya Arusha, Mwenge wa Uhuru 2019, umetembelea na kukagua miradi 8 yenye thamani ya shilingi bilioni 15.9 kwenye sekta za elimu, afya, maji, mifugo na uwekezaji, huku miradi mitatu imewekwa jiwe la Msingi, miradi miwili imezinduliwa na kukagua miradi mitatu.
Picha za matukio ya Mweng wa Uhuru 2019.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2019,ndugu Mzee Mkongea Ali, akiweka Jiwe la Msingi jengo la mama na mtoto, hospitali ya Olturumet.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2019,ndugu Mzee Mkongea Ali, akipanda mti kwenye shule ya sekondari Oldonyowas wakati akizindua shule hiyo.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2019, ndugu Mzee Mkongea Ali, akiweka Jiwe la Msingi kuzindua mradi wa ufugaji Nyuki Oldonyowas.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.