Na Elinipa Lupembe
Wananchi hususani watoto na wazazi wa Kijiji cha Bwawani na vitongoji vyake, kata ya Bwawani halmashauri ya Arusha, wailaya ya Arumeru, wamemshukuru mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea madarasa kwenye shule ya Msingi shikizi ya Olokii katika kitongoji cha Olmapinuu.
Wananchi hao, wamefikia hatua hiyo mara baada ya serikali kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni 101 kwa awamu mbili za ujenzi wa miundombinu ya shule shikizi, ikiwemo vyumba 2 vya madarasa, matundu 10 ya vyoo na nyumba ya mwalimu na tayari wanafunzi wanaendelea na masomo shuleni hapo.
Mkuu wa Idara ya Mipango, halmashauri ya Arusha, Anna Urio, amefafanua kuwa, fedha hizo zimekuja kwa awamu mbili, mishoni mwa mwaka 2021 serikali ilitoa milioni 40 fedha za UVIKO 19, zilitumika kujenga vyumba 2 vya madarasa na madawati 25 na mwaka 2022 ikitoa shilingi milioni 61, milioni 50 za ujenzi wa nyumba ya walimu na milioni 11 za ujenzi wa matundu 10 ya vyoo vya wanafunzi.
Aidha katika utekelezaji wa ujenzi wa nyumba ya mwalimu, wananchi wa kijiji cha Bwawani wamejikuta wakisukumwa kuongeza nguvu kazi katika utekelezaji wa miradi hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa watoto na walimu wao.
Wakizungumza na mwandishi wetu, wananchi waliokuwa wakisaidia mafundi kujenga nyumba ya mwalimu, wamebainisha kuwa wamefikia hatua hiyo, kutokana na kuona umuhimu wa nyumba hiyo ya walimu, nyumba ambayo walimu wataishi hapo na kuwafundisha watoto wao.
Mjumbe wa kamati ya Mapokezi ya Ujenzi, Shaban Rashid amesema kuwa, watoto wao wamekuwa wakiteseka kwa miaka mingi, kutokana na shule ya msingi kuwa mbali na kutenganishwa na korongo ambalo wakati wa mvua watoto hushindwa kuvuka na kukosa masomo kwa zaidi ya miezi 4 mpaka 6 wakati mwingine.
"Tunamshukuru mama Samia, kweli amekikumbuka kijiji chetu hasa kitongoji cha Olmapinuu, kitongoji ambacho watoto wengi waliacha shule kwa kukata tamaa ya umbali na wengine kucheleweshwa kuandikishwa shule kutokana na wazazi kuhofia madhara watakayokutana nanyo njiani hasa kipindi cha mvua". Amefafanua Ally.
Aidha ameipongeza serikali kwa kuwashirikisha wananchi katika usimamizi wa miradi, jambo ambalo linawafanya wananchi, kumiliki miradi lakini linawafanya kujihakikishia matumizi sahihi ya pesa zao za Umma.
Hata hivyo wanafunzi wa shule hiyo shikizi, wameipongeza na kuishukuru serikali na kudai kuwa kwa sasa wanasoma kwenye madarasa mazuri, na watoto wengi wanapata fursa ya kuanza shule kwa wakati.
Yunus Alley mwanafunzi wa darasa la awali, amesema kuwa kwa sasa wanasoma kwa furaha, madarasa ni mazuri, shulemiko karibu na nyumbani.
Akitoa ushuhuda wa kuanza kwa shule hiyo mwalimu Zakayo Lukumai, ameema shule ilianza mwka 200 kwa wanafunzi kukaa chini,na baadaye kupata darasa la nyasi, mwaka 2022 serikali imejenga madarasa mawili mazuri, madarsa ambayo yamesababisha ongezekomla wanafunzi shule hapo.
"Kwa sasa tuna ongezeko la wanafunzi, wamefikia 110, kutoka wanafunzi 40 hapo awali, kwa sasa wazazi wamepata mwamko wa kuwaandikisha watoto kuanza shule". Amesisitiza Mw. Lukumai
Awali Serikali inandelea na mkakati wa kuboresha miundo mbinu ya shule ili kuhakikisha watoto wenye umri wa kwenda shule, wanaandikishwa kwa wakati.
ARUSHA DC
KaziInaendelea✍
PICHA ZA WANAFUNZI WAKIWA DARASANI NA MAENDELEO YA UJEZNI WA NYUMBA YA MWALIMU NA VYOO
Wanafunzi wa darasa la kwanza shule shikizi ya Olokii kitongoji cha Olmapinuu kijiji cha Bwawani, wakifurahia masomo baada ya serikali kujenga mdarasa mazuri shukeni hapo.
Wananchi wakisaidia mafundi ujenzi wa nyumba ya mwalimu
,
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.