Elinipa Lupembe.
Wananchi wa kijiji cha Olimringaringa kata ya Kimnyaki, halmashauri ya Arusha, wameiomba serikali kubadilisha matumizi ya ardhi, katika eneo la serikali lililokuwa likitumika kama josho la kuoshea mifugo kijijini hapo, badala yake, eneo hilo litumike kujenga Kituo cha afya.
Wananchi hao wametoa rai hiyo, mbele ya wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango wa halmashauri hiyo, wakati wakiwa kwenye ziara kukagua miradi ya maendeleo na maeneo ya umma kijijini hapo.Wananchi hao wameweka wazi kuwa, historia ya eneo hilo, lilikuwa likitumiwa na wafugaji kuogeshea mifugo yao, lakini kwa miaka mingi sasa eneo hilo halitumiki, kutoka na wafugaji wengi sasa, kuhamia kwenye ufugaji wa kisasa, wa kifuga ndani, ambapo kila mfugaji humudu kuosha mifugo yake nyumbani.
Wamethibitisha kuwa, josho hilo kwa muda mrefu sasa halitumiki, wao kama wanakijiji wameendelea kulitunza eneo hilio kwa muda mrefu, na kuongeza kuwa, imefika wakati wanaomba kubadilisha matumizi, ili eneo hilo liweze kutumika kwa shughuli nyingine za kijamii, kuliko kubaki bila kutumika kwa muda mrefu.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Kijiji cha Olimringaringa Mheshimiwa, Wilson Emanuel, aliuomba uongozi wa halmashauri kufanya ukarabati wa josho hilo, lakini baadhi ya wananchi walipinga hoja hiyo na kuomba eneo hilo, kujengwa kituo cha afya, kutoka na ukweli kwamba kwa sasa wafugaji wengi wamebadilisha mfumo wa ufuagi ambao, kila mfugaji humudu kuhudumia mifugo yao nyumbani, tifauti na hapo awali.
Naye Eliakim Kilusu, mkazi wa kijiji cha Olmringaringa, amethibitisha kuwa kata ya Kimnyaki haina Kituo cha afya na wananchi wa eneo hilo, hulazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya, na kusisitiza kuwa, ni vema eneo hilo likabadlishwa matumizi na kujenga kituo cha afya.
"Kipaumbele chetu kwa sasa ni kuwa na kituo cha afya katika eneo hili, kwa kuwa hatuna zahanati, watu wanapata shida na kutumia gharama kubwa, pindi wanapougua hasa nyakati za usiku, kufuata huduma za afya vijiji vya jirani, ambapo kuna umbali mrefu" amesisitiza Kilusu.
Akijibu hoja za wananchi hao, Makamu Mwenyekiti, halmashauri ya Arusha na Diwani wa kata ya Mateves, mheshimiwa Freddy Lukumay, licha ya kuwapongeza wanachi hao kwa kutunza eneo hilo kwa muda mrefu, amewaagiza viongozi wa kijiji hicho, kufanya mkutano wa wananchi wote, ili wakubaliane kile wanachohitaji serikali yao kufanya katika eneo hilo na kumuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha na timu yake ya watalaamu, kusimamia ombi la maamuzi yatakayoletwa na wananchi hao wa Kimnyaki.
Naye Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, ameahidi kutegeleza agizo hilo kwa kuzingatia matakwa na maamuzi yatakayofanywa na wanachi hao wa Kimnyaki, kupitia vikao na mkutano wa kisheria na kuliwasilisha ofisini kwake.
"Niwapongeze pia kwa kutunza eneo hili, na sio kulitunza tu, zaidi kwa kuwa na hati miliki ya kimila, jambo ambalo vijiji vingi vinamiliki maeneo bila kuwa na hati, fanyeni maamuzi ya nini mnahitaji kwa kuzingatia kipaumbele cha huduma mnayohitaji, pamoja na kufuata taratibu za vikao na mkutano wa kisheria, halmashauri na timu ya watalamu tutafanyia kazi maamuzi yenu kwa wakati na kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu" . Amesisitiza Msumi
Awali wajumbe hao wa Kamati ya Fedha, wamefanikiwa kutembelea miradi 9 ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na eneo hilo la wazi linalomilikiwa na serikali kupitia Idara ya mifugo lililoko kijiji cha Olmringaringa kata ya Kimnyaki.
ARUSHA DC
KaziInaendelea✍✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.