Kama ilivyokawaida ya wananchi wengi katika karne hii kuwa na shauku ya kupata maendeleo katika maeneo yao hata kwa kuchangia kiasi cha fedha, mali na hata nguvu zao ikiwa ni lengo moja kubwa la kuhakikisha huduma zote za jamii zinapatikana kwa urahisi katika maeneo wanayoishi.
Hali hiyo imejitokeza mubashara kwa wakazi wa Kitongoji cha Ekenywa kata ya Olturumet walipofanya mkutano mkuu wa kitongoji hicho kwenye viwanja vya shule ya Msingi Ekenywa na kukutana na Timu ya watalamu watekelezaji wa mradi wa maji wa vijiji vitano mradi unaotekelezwa na shirika la waterAid Tanzania kwa ufadhili wa Idara ya Maendeleo Uingereza 'DFID'
Wananchi hao wameonesha ari kubwa ya kutaka mradi huo uanze hata kesho kwa kuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa maji katika eneo hilo na kusababisha wananchi hasa wanawake kutumia muda mrefu kutafuta maji jambo ambalo linapoteza muda wa kulijenga taifa na kuchelewesha maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.