WANANCHI WA KIJIJI CHA MLANGARINI NA KISERIANI WAISHUKURU SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUZIKOMBOA KAYA MASIKINI
Wananchi wa Kijiji cha Mlangarini pamoja na Kiseriani wameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan jinsi inavyoonyesha kwa Vitendo kuzikomboa kaya Masikini.
Wakizungumza wakati wa kupokea fedha hizo leo Tarehe 07 Novemba 2024 wananchi hao waliokuwa katika kijiji cha Mlangarini na Kiseriani Halmashauri ya Wilaya ya Arusha ambao ni wanufaika wa fedha za kusaidia kaya Masikini zinazo simamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF). Wamesema kupitia fedha hizo wamejiinua kiuchumi kwa kununua biashara ndogondogo, kilimo na ufugaji kwenge maeneo yao.
Akizungumza kwa niaba ya wanufaika wenzake wa kijiji cha Mlangarini ambapo fedha hizo zimewasaidia kusomesha watoto wao kupitia biashara ndogo ndogo, kilimo na ufugaji amesema wanatoa shukrani kwa Rais Samia kwa uamuzi wake wa kutoa fedha hizo na kuwafikia moja kwa moja wahusika na hivyo kubadili Maisha yao.
“Tunashukuru Serikali ya Rais Samia kwa Mpango huu kwakuwa umetusaidia Sisi kaya Masikini kupitia fedha hizo tumeanzisha biashara ndogo ndogo, tunafanya ufugaji wa kuku na tunafanya kilimo, vile vile tunawasaidia watoto wetu kuwanunulia vifaa vya shule na zaidi tunanunua chakula kwa hili Tunasema Asante Rais samia”
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.