• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wananchi wa Ngaramtoni kutumia mila ya kuvunja chungu, kusaka wezi wa vifaa vya maji

Posted on: June 27th, 2018

Na. Elinipa Lupembe.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida wananchi wa vitongoji vya Ngaramtoni na Emaoi kata ya Olmotony wameamua kutumia njia za kimila kuwatafuta wahalifu, walioiba vifaa kwenye miundombinu ya vituo vya kuchotea maji.

Kufuatia uharibifu na wizi wa vifaa hivyo, wananchi wamekubaliana kwa pamoja, kutafuta wezi hao kwa kutumia mila na desturi zao kimasai katika mkutano wa hadhara, uliojumuisha wananchi  wa vitongoji hivyo, uliofanyika kwenye viwanja vya CCM Ngaramtoni.

Wananchi hao baada ya majadiliano yaliyokuwa na hisia za kusikitishwa kutokea kwa vitendo hivyo vya kihalifu katika maeneo yao, wametoa kutoa siku saba kwa mtu au kikundi cha watu, waliohusika na wizi huo,kurudiasha vifaa hivyo na endapo havitarudishwa taratibu za kimili zitafuatwa.

Wananchi hao wamebainisha kuchoshwa na kusikitishwa na wizi mdogomdogo, unaoendelea katika jamii yao pamoja na tabia mbaya iliyojitokeza ya kuiba, hadi vifaa vilivyowekwa na wafadhili kwa ajili ya kuwaihudumia jamii yao.

Aidha wananchi hao wameonesha kuchukizwa na tukio hilo la wizi kwa kuwa mradi huo umegharamiwa na wafadhili kupitia serikali yao na kukiri kuwa mradi huo ni kwa faida yao, hivyo ni bora kuvunja chungu ili kukomesha tabia hiyo.

"Sisi wananchi wa Ngaramtoni tumechoshwa na adha ya maji, leo mfadhili kajitokeza ili tupate huduma ya maji, watu wanaharibu na kuiba vifaa, hatutakubaliana na tabia hiyo na ili kuikomesha tuvunje chungu" wamesema wananchi hao.

Akitangaza makubaluano hayo,Mwenyekiti wa kitongoji cha Emaoi Mh. Obed Kaipuk ametoa siku saba kwa wananchi kurudisha vifaa hivyo au kwa mtu yoyote aliyeona au kufahamu wahalifu hao na kuwataja kwa siri. 

Ameongeza kuwa endapo siku saba zitapita bila wahalifu hao kujitokeza, siku ya tarehe 04.07. 2018, viongozi watakutana na wazee wa mila na kufanya taratibu za kuvunja chungu hicho.

Naye, Esuvati Meikara, mkazi wa kitongoji cha Ngaramtoni amethibitisha, kuwa kupitia imani ya kabila la kimasai ya kuvunja chungu, ni lazima wahalifu hao watajitokeza na kurudisha vifaa hivyo, na kila mmoja atakuwa mlinzi wa miundombinu hiyo ya maji.

Awali mratibu wa mradi wa shirika la WaterAid Arusha na Manyara, Upendo Muntambo, amesema kuwa licha ya kuharibu miundo mbinu hiyo lakini wezi hao wamefanikiwa kuiba betri na sola kwenye vituo sita, vifaa vinavyokadiriwa kuwa na  thamani ya shilingi milioni sita.

Uongozi wa halmashauri ya Arusha, unawataka wananchi wote kuthamini na kuilinda miradi yote inayotekekezwa na serikali, kwenye maeneo yao pamoja na kutambua kuwa miradi hiyo ni mali ya umma na si mali ya mtu yoyote binafsi.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.