Na Mwandishi Wetu.
Wananchi wa halmashauri ya Arusha wametakiwa kuwa watulivu na kuepuka upotoshaji juu ya usitishwaji wa mikopo ya asililimia 10 ya mapato ya ndani iliyokuwa ikitolewa kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye walemavu na kusitishwa kwa muda huku serikali ikiendelea kufanya maboresho ya namna bora ya utoaji na urejeshaji wa mikopo hiyo.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman msumi wakati akijibu swali lililoulizwa na Diwani wa viti maalum - CCM, Mhe. Anneth Kifwe aliyetaka ufafanuzi juu ya mkakati wa halmashauri kutoa elimu kwa wananchi kutokana na tamko la Serikali kusitisha kwa muda mikopo ya asilimia 10 ili wananchi waweze kuepukana na upotoshaji unaondelea na baadhi ya taasisi za kifedha kwenye vijiji na vitongoji vyao, wakati wa Mkutano cha Baraza la Madiwani cha robo ya nne mwaka wa fedha 2022/2024 uliofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo.
Mkurugenzi Msumi amesema kuwa, serikali ilisitisha utoaji wa mikopo isiyo na riba inayotolewa na halmashauri kupitia ahsilimia 10 ya mapato ya ndani mikopo hiyo isiyo na riba ilisitishwa kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza ili kufanya tathmini na maboresho na hatimaye kuja na njia bora zaidi ya utoaji na urejeshaji wa mikopo hiyo sambamba na kuwafikia walengwa wenye sifa."Changamoto zilizojitokeza ni badhi ya vikundi kuchukua mkopo na kupuuzia kurejesha kwa wakati na wengie kutokurejesha kabisa kwa kuona ni fedha za Serikali jambo ambalo lilisababisha hasara na malengo ya utoaji wa mikopo hiyo kutokutimia, Serikali baada ya kuona changamoto hiyo kupitia ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali iliamua kusitisha mikopo hiyo kwa muda ili kutafuta namna bora ya kuendelea kutoa mikopo hiyo ili wananchi waendelee kunufaika na kujikwamua kiuchumi." Amebainisha Mkugenzi Msumi.Hata hivyo amewasisitiza wanaanchi kuwa wavumilivu na kuachana na mikopo inayotolewa na mTaasisi za kifedha yenye riba kubwaa kwa kuwa, utoaji wa mikopo isiyokuwa na riba utarejea, na kuongeza kuwa, halmashauri inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Watendaji wa vijiji na Kata hadi pale utaratibu wa serikali wa kurejesha mikopo hiyo utakaporejeshwa na wananchi kuendelea kunufaika na mikopo
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Arusha, Stedvant Kileo amewataka waliokopeshwa fedha hizo waendelee kufanya marejesho kama kawaida ili fedha hizo ziendelee kuwanufaisha wananchi wengine kwani serikali haijasitisha utaratibu wa kufanya marejesho kwa vikundi vilivyokuwa vimekopeshwa hapo awali.
Ameongeza kuwa, wananchi waliokopeshwa mikopo hiyo wanapaswa kuendelea na shughuli zao za uzalishaji na kupuuza upotoshaji kutoka kwa watu na taasisi zisizokuwa na vibali maalum kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wenye lengo la kupotosha dhana ya serikali kwani utaratibu utakapokamilika wa utoaji wa mikopo hiyo wananchi watajulishwa kupitia mamlaka husika.
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.