Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, anawakaribisha wananchi wote kutembelea Mabanda la Halmashauri ya Arusha, kwenye Maonesho ya Wakulima Nane Nane yaliyoanza tarehe 01 -8 Agosti, 2020, kwenye viwanja vya Nanenane Njiro.
Wananchi wote Wakulima na Wafugaji MAALIKWA Kutembelea kwenye Banda halmashauri ya Arusha kujionea shughuli mbalimbali za Kilimo na Mifugo na kujifunza mambo yafuatayo:-
-: Kilimo cha mbogamboga kinachoendana na matumizi bora ya Ardhi kwa maeneo ya mijini, badala ya kupanda maua, utajifunza kupanda mbogamboaga za aina zote kama urwmbo wa nyumba.
-: Uatakutana na watalamu wa Kuelekeza kanuni za Kilimo bora kwa kutumia pembejeo bora za Kilimo ikiwemo uchaguzi wa mbegu bora, matumizi ya mbolea ya kupandia na kukuzia.
-: Kutana na watalamu watakao kuunganisha Mkulina na Mfugaji na Mfuko wa Pambejeo wa Taifa uweze kukopa zana za kilimo ikiwemo Matrekta, mashine zote za Kilimo pamoja na shughuli zote za Umwagiliaji.
-: Kutana na watamu wa Lishe bora watakaokuwezesha kuongeza thamani kwenye mazao ya Kilimo na Mifugo, kuandaa na kuhifadhi chakula.
-: Kutana na watalamu wa Kilimo na Ushirika, namna ya kuanzisha SACCOS na Vyama vya Msingi (AMCOS).
-: Utakutana na watalamu wa Afya na mobile Clinic pale utapata huduma za upimaji wa Ugonjwa wa UKIMWI, Tathmini ya Lishe kwa kupima uzito kuendana na urefu wako.
KAULI MBIU 2020:
"KWA MAENDELEO YA KILIMO, UFUGAJI NA UVUVI CHAGUA VIONGOZI BORA"
PICHA ZA BANDA LA HALMASHAURI YA ARUSHA.
Banda la Kilimo la Halmashauri ya Arusha kwenye viwanja vya Nane Nane Themi - Jijini Arusha.
Kilimo cha nyumbani cha mbogamboga kwenye maeneo ya mjini, otesha mboga badala ya maua nyumbani.
Kilimo cha nyumbani cha mbogamboga kwenye maeneo ya mjini, otesha mboga badala ya maua nyumbani.
Pembejeo za Kilimo, ikiwemo mbegu bora za mazao, mbole za kupandia na kukuzia.
Mobile Clinic Car, huduma za Afya zinapatikana hapo bila malipo yoyote, huduma ya vipimo vya Virusi vya UKIMWI, Tathmini ya Lishe kwa kupima uzito na urefu na kupata ushauri wa kudhibiti uzito uliozidi.
Afisa Lishe halmashauri ya Arusha Doto Milembe (kulia) akimpima urefu mmoja wa vijana (jina kapuni) aliyefika kwenye banda la halmashauri ya Arusha kupata ushauri wa Afya na Lishe kudhibiti uzito uliozidi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.