Na Elinipa Lupembe
Wananchi wilaya ya Arumeru, wanaojishughulisha na kilimo haramu cha bangi, wametakiwa kuacha mara moja kilimo hicho huku serikali ikiwa na mkakati wa kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kutaifisha mashamba na mali zao, endapo watabainika kuendelea na kilimo hicho cha bangi.
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda, wakati wa oparasheni maalumu ya kutokomeza kilimo cha bangi kijiji cha Kisimiri Juu, ikiwa ni oparesheni ya kitaifa ya kupiga vita na kutokomeza madawa ya kulevya nchini.
Katika operesheni hiyo, iliyoongozwa na Mkuu wa wilaya ya Aruemru, pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya, jumla ya magunia 270 ya bangi na Kilo 300 za mbegu zilikamatwa na kuteketezwa kwa moto huku watuhumiwa wanne wakikamatwa na kuchukuliwa na Jeshi la Polisi.
Hata hivyo Mkuu huyo wa wilaya amesikitishwa na kitendo cha wananchi wa kijiji hicho kufuta namba za anwani za makazi zilizowekwa na serikali kwenye nyumba zao, jambo ambalo linawafanya kushindwa kutambua rasmi miliki halisi wa nyumba ambazo magunia ya bangi yanakutwa ndani ya nyumba hizo ni ya nani.
Aidha ameweka wazi mkakati wa serikali sasa ni kurasimisha mashamba yote ya wananchi wa kijiji hicho ili kuweza, hati miliki na kutambua mmiliki halisi na halali wa shamba na kurahisisha utambuzi wa mtu anayelima bangi kwenye shamba husika.
"Serikali kupitia Mamlaka ya kudhibiti Madawa ya Kulenya wamekuwa waktoa elimu kwa wananchi kuacha kulima bangi lakini bado wapo baadhi ya watu wanakaidi na kuendelea na kilimo hicho haramu, tumekamata magunia 270 na Kilo 300 za mbegu za bangi jambo ambalo linaashiria bado kilimo hicho kinafanyika sana katika vijiji vya Kisismiri Juu na Losinoni Juu" Amesisitiza Mhe. Mkuu wa wilaya huyo.
Naye Mwakilishi wa Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kuupambana na Dawa za kulevya, Afisa Operationi Jackson George, amesema kuwa licha ya Mamlaka hiyo kutoa elimu ya sababu za kuzuia kilimomna matumizi ya bangi lakini bado wanachi wa Kisimiri wanaendelea kulima na kuuza zao hilo kwa siri, lakini Serikali itaendelea kutoa elimu na kuchukua hatua kali za kisheria kwa yeyote atakayebainika.
Operasheni ya kutokomeza kilimo cha bangi inaendelea, katika wilaya ya Arumeru hukue serikali ikiwa na mikakati thabiti ya kahakikisha wananchi wa Kijiji cha Kisimiri Juu na Chini halmashauri ya Meru na Kijiji cha Losinoni Juu halmashauri ya Arusha wanaachana na kilimo cha bangi.
ARUMERU BILA BANGI INAWEZEKANA
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.