Wanaume wametakiwa kushirikiana na familia zao kuhakikisha, zinapata chakula bora ili kukabiliana na changabmoto ya utapiamlo hususani kwa watoto wa chini ya miaka mitano.
Hayo yamesemwa wakati wa kikao cha tathmini ya Lishe cha robo ya nne mwaka wa fedha 2022/2023, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.
Katika kikao hicho kilichoongozwa na Afisa Tarafa ya Moshono Dominick Njuriwa, kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Arumeru, imeoneka baadhi ya kinababa hawashiriki katika malezi ya watoto na kuwaachia kina mama wakiteseka na familia jambo ambalo linasababisha watoto kukosa chakula na kusababisha kuwa na utapiamlo.
Mwenyekiti huyo, amewataka wanaume kuwacha tabia ya kutelekeza familia badala yake kuwahurumia kina mama na watoto kwa kushirikiana katika malezi na kuhakikusha watoto wanapata chakula bora kwa kuwa ndio msingi wa makuzi ya akili na mwili wa mtoto.
Aidha amewataka watalamu kuendelea kuelimisha jamii, umuhimu wa malezi na upatikanaji wa chakula bora kwa familia, huku akiwataka watendaji kuona namna ya kuwachukulia hatua, wanaume wanaotelekrza familua zao kupitia
ofisi za Ustawi wa Jamii.
Afisa Mtendaji kata ya Sambasha, Peter Chimwelo, amesema kuwa katika kata hiyo, wanaume wamekuwa wakiacha familia zao na kwenda kufanya kazi nchini Kenya, na kuwaacha kinamama wakizihudumia familia jambo ambalo wanaelemewa na kushindwa kukidhi mahitaji ya familia kwa kukosa chakula bora.
"Wanaume wanaenda Kenya kufanyakazi, wanaziacha familia kwa muda mrefu, kina mama wanaelemewa na majukumu, wakati mwingine kushindwa hata kupata chakula cha watoto, na kusababisha utapiamlo". Ameweka wazi Chimwelo
Naye Afisa Mtendaji kata ya Musa Justina Mugera amesema kuwa, kata hiyo watu hulima zao la tumbaku zaidi, baada ya mavuno wanaume ndio wenye haki na dhahnauna yae kuuza, baada ya mauzo hawakubuki kununua chakula cha kutosha cha familia, na kusababisha watoto kukosa chakula na kupata utapuamlo.
"Licha ya kwamba elimu inatolewa bado kuna changamoto kubwa kwa baadhi ya familia inayotoka na mila za mfumo dume, kina mama ndio wakulima na watunzaji wa mashamba, mazao yaikivunwa, mama hausiki tena, hii inasababisha familia kukosa chakula, kwa kuwa baba ndiyo mmiliki wa pesa, hakumbuki tena familia na baadhi huhama nyumbani kwa muda". Amefanua Jestin.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.