Na. Elinipa Lupembe.
Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani 2020, yamefanika kwenye kijiji cha Engalaoni kata ya Mwandeti na Kijiji cha Lemanyata kata ya Olkokola, huku wanaume wakijitokeza kwa wingi na kukiri kupata uelewa mkubwa wa umuhimu wa kumuwezesha mwanamke kumnyonyesha mtoto miezi 6 ya mwanzo bila kumoa chakula kingine.
Aidha wamekiri kufahamamu faida za kumnyonyesha mtoto miezi sita ya mwanzo bila kumpa chakula kingine ikiwa ji pamoja na kuimarisha kinga ya mwili itakayo mkinga mtoyo kushambuliwa na maradhi, kuimarisha mwili wa mtoto katika makuzi, kumfanya mama kuzingatia
Lakini pia wanaume hao, wafahamu madhara makubwa yanayoweza kumpata mtoto asiponyonyeshwa kwa utaratibu, ikiwemo kuharibu mfumobwa mmeng'enyo wa chakula kwa mtoto,udumavu wa mwili na akili kwa mtoto.
Hata hivyo wanaume hao, wamesema wako tayari kushirikiana na mwanamke katika kipindi chote cha ujauzito, kujifungua na kipindi cha siku 1000 za kunyonyesha, sambamba na kumuwezesha mama kupata lishe bora ili mtoto apate maziwa yenye virutubisho vya kutosha kwa afya ya mtoto na jamii,mkwa maendeleo ya Taifa.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.