• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wanufaika wa mpango wa TASAF wa kunusuru kaya masikini wajipanga kuelekea ukomo wa mradi

Posted on: June 29th, 2019

Na. Elinipa Lupembe.

Wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini, halmashauri ya Arusha, mpango unaotekelezwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii - TASAF awamu ya III, wameanza mkakati wa kujipanga kuondokana na umasikini uliokithiri, uliokuwa ukizikabili kaya hizo, kuelekea kufikia ukomo wa mradi huo.

Mwandishi wa habari hizi, alipata fursa ya kukutana na kuzungumza na vikundi vitano, vinavyotokana na wanufaika wa mpango huo wa kunusuru kaya masikini, katika kijiji cha Engorora kata ya Kisongo, wakati wa semina elekezi ya kuwajengea uwezo, wa kuboresha shughuli za kuweka na kuwekeza fedha kupitia kikundi.

Wanufaika hao, wamethibitisha kuwa, wamekuwa  wakipatiwa mafunzo ya kuweka na kuwekeza fedha, wanazopata kutokana na mpango na zile wanazopata kutokana na shughuli zao nyingine, kwa lengo la kuwa na fedha kwa ajili ya dharura na vipindi vigumu vya maisha, pamoja na kuanzisha shughuli mbalimbali za kuongeza kipato cha kaya zao.

Wamesema kuwa, licha ya serikali kupitia TASAF kuwapa fedha za ruzuku za mpango wa kunusuru kaya masikini, lakini pia imeweza kuwajengea uwezo wa kuanzisha vikundi vya kuweka na kukopa, vikundi ambavyo vimewawezesha kuanzisha shughuli mbalimbali za kuinua kipato, ikiwemo kilimo, mifugo na biashara ndogondogo.


Naitanamwang'aik Sambwete, Mwenyekiti wa kikundi cha Erereto, amesema kuwa, kwa sasa, wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini, wameanza kujiwekea mikakati ya kujikwamua kiuchumi, kupitia vikundi vyao vya kuweka na kukopa, vikundi ambavyo vinawapa fursa ya kukopeshana fedha na kupata mitaji ya kuanzisha shughuli mbalimbali za kibiashara.

Naitanamwang'aik ameeleza kuwa, kikundi chao kilianza mwaka jana, mwezi Juni, 2018 kikiwa na wanachama 15, kwa kuweka akiba ya shilingi 2,500 kila wiki, na kukopeshana kwa riba ya asilimia 5, na baada ya miezi 12, waliweza kugawana kiasi cha shilingi 182,500, kwa faida ya shilingi 62,500 kwa kila mwana kikundi.

Amethibitisha kuwa licha ya faida hiyo ya elfu 62 kwa mwaka, zaidi wanakikundi walipata fursa ya kukopa na kuanziasha shughuli za uzalishaji pamoja  kutatua matatizo ya kifamilia ikiwemo matibabu, kulipa karo na kununua mahitaji ya familia zao.

Hata hivyo kikundi hicho kimeweka mkakati wa kuchanga shilingi 5,000 kila mwezi na kuanza kumnunulia mwanakikundi mmoja mbuzi wa maziwa, na wanategemea baada ya miezi 15, kila mwanakikundi atakua na mradi wa mbuzi wa maziwa, mradi ambao wanaamini utaongeza pato la familia.

Esuvat Levosu wa kikundi cha Upendo, ameshuhudia  kuwa, tangu mradi huo wa TASAF, kuwajengea uwezo wa kuanzisha vikundi vya kuweka, kuwekeza na kukopeshana, wameweza kuzikwamua  familia zao  kiuchumi, tofauti na hapo awali, maisha ya familia zao yalikuwa magumu na yasiyokuwa na mwelekeo.

" Familia zetu zilikua na maisha ya kuunga unga, maisha ya kubahatisha na yasiyo na mwelekeo, kupitia vikundi vyetu, tunauhakika wa kuendesha maisha ya familia zetu, na tumeanza kuweka mikakati ya muda mrefu, hata mradi wa masikini ukiisha tutakuwa na shughuli za kutuingizia pesa" amesema Esuvati.

Katibu wa Kikundi cha Meseyeki, Febronia Buani, amesema kuwa, tangu tumeanza kuwa na kikundi cha kuwekeza na kukopeshana, ameweza koboresha mradi wake wa ng'ombe wa maziwa, kwa kukopa fedha zilizomsaidia kununua chakula bora cha mifugo yake na kumfanya kufuga kisasa zaidi, huku ng'ombe hao wakitoa maziwa mengi tofauti na hapo awali alikua alifuga kienyeji.

"Nilikuwa nafuga ng'ombe lakini sikuwa na uwezo wa kufuga kisasa, tangu nimejiunga kwenye kikundi cha kuweka na kuwekeza fedha,nimeweza kukopa na kuboresha mradi wangu wa ng'ombe wa maziwa, kwa kutumia fedha hizo kufuga kisasa, nanunua pumba, majani, virutubisho na kuwatibu ng'ombe wangu kwa wakati pindi wanapougua, ng'ombe ni wazuri na wameanza kutoa maziwa mengi zaidi kwa sasa" amethibitisha Fabiola

Aidha Fabiola ameongeza kuwa, wamekuwa wakishauriana shughuli za kufanya kama wanakikundi ili kuweza kujipatia kipato, pamoja na kufuatiliana kuhakikisha kila mwanakikundi ameanzisha au kuendeleza shughuli ya kuingiza kipato, huku wakifuatilia zaidi matumizi sahihi ya fedha ambazo mwanakikundi amekopa ili aweze kurejesha na kuepuka matumizi tofauti ya fedha hizo.

Awali, Mratibu wa TASAF mkoa wa Arusha, Mathias Seif, amefafanua  kuwa, lengo la Serikali ni kuhakikisha walengwa wote wa mpango wa kunusuru kaya masikini, ni kuwa na shughuli rasmi za kuwaingizia kipato, shughuli ambazo zitaimarisha uchumi wa kaya kwa wakati wote, hata mradi utakapofikia ukomo.

Ameongeza kuwa, TASAF imekuwa ikitoa mafunzo ya mara kwa mara kwa vikundi hivyo, lengo likiwa kuwajengea uwezo wa kuweka akiba na kuwa na fedha za kutumia wakati wa vipindi vigumu, pamoja na kuwekeza fedha kwa ajili ya kukopeshana na kuanzisha shughuli endelevu za kuwaingizia kipato, ili kuondokana na umasikini uliokithiri kuelekea uchumi wa kati ifikapo 2025.




Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA August 14, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • KUFUATILIA NA USAMIZI WA HAKI ZA MTOTO KATIKA JAMII NI JAMBO MUHIMU

    August 25, 2025
  • RAIS SAMIA AMUAPISHA AMOS MAKALLA KUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA

    August 26, 2025
  • DKT. JAHANNES LEMBULUNG' LUKUMAY ACHUKUWA FOMU YA UGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI

    August 25, 2025
  • KIKAO KAZI CHA WENYEVYITI WA BODI NA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI ZA UMMA (CEOs Forum 2025)

    August 24, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.