Na. Elinipa Lupembe.
Kaya zinazonufaika na Mpango wa Kunusuru kaya Maskini kijiji cha Oldonyowas, halmashauri ya Arusha, mradi unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF awamu ya III, wamekiri kaya hizo kuanza kuondokana na umasikini uliokithiri kwa kujimudu kimaisha kupitia biashara ndogondogo wanazozifanya, zinasaidia kuongeza pato la kaya.
Wakizungumza kwa niaba ya kaya hizo zinazonufaika na mradi huo wa kunusu kaya maskini ,mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za mitaa, wanakaya hao licha ya kuishukuru na kuipongeza serikali, wameweka wazi kuwa kupitia miradi inayofanyw a na TASAF kijijini hapo, zile kaya ambazo zilikuwa maskini sana, zimeanza kubadilika na kuanza kuwa na mpango wa endelevu wa kujiongezea kipato, tofauti na hapo awali, kaya hizo ziliishi maisha ya kubahatisha.
Lucy Wiliam, mlengwa wa kaya maskini amesema kuwa, mradi wa kupokea pesa za ruzuku pamoja na kupatiwa elimu ya ujasiriamali kupitia vikundi vya wekeza vya kinamama wanufaika wa mradi, wameweza kuweka pesa na kukopeshana, pesa ambazo zimewapa mitaji ya kufanya biashara mbalimbali ikiwemo za mazao ya mboga mboga, ufugaji wa kuku, mbuzi na kondoo, jambo ambalo limeinua kipato cha kaya nyingi na kuzifanya kaya hizo kumudu kupata mahitaji muhimu ya familia
"Wananchi wa Oldonyosambu kwa sasa hawana tofauti na wale wa Dar es salama, watoto wetu wanapata mahitaji yote kama watoto wa mjini, kwa sasa tunauwezo wa kuendesha biashara ndogo ndogo ambazo zinatuwezesha kumudu kukidhi mahitaji ya familia kama chakula cha watoto, tunanunua mahitaji ya shule ya watoto, tunalipa ada za watoto, yaani TASAF imefanya na sisi watoto wetu kusoma vizuri kama watoto wengine" amesema Lucy.
Hata hivyo wajumbe hao, wamewapongeza wana kaya hao, kwa kuwasistiza kuwa serikali inapata ari ya kuendelea kusaidia jamii, pale ambapo jamii inapokea miradi na kuitekeleza kwa ustadi kama ilivyo kwa wanachi wa Oldonyowas, wanachi ambao wanafikisha serikali kwenye kusudio lake na kuwasisitiza kuendelea kuunga mkono juhudi hizo za serikali kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuondoa umaskini uliokithiri nchini.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya kudumu ya Bunge Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdala Kalembo, amesema kuwa, lengo la miradi ya TASAF ni kuondoa umaskini uliokithiri kuanzia ngazi ya kaya, na kuwapongeza wana kaya hao kwa kutekeleza kwa vitendo adhma hiyo ya serikali na kuwataka kuendelea kushirikiana na serikali kupambana na umaskini uliokithiri katika kaya zao.
"Inaridhisha sana pale unapokuta wananchi wameimiliki miradi inayotekelezwa na serikali kama ilivyo kwa wananchi hawa wa Oldonyowas, kwa kufanya hivi serikali itafikia malengo yake ya kuondoa umaskini kwenye jamii na taifa kwa ujumla" amesisitiza Mheshimiwa Bulembo.
Tangu mwaka 2014, TASAF awamu ya III na mpango wa kunusuru kaya masikini, imetekeleza katika vijiji 45 vya halmashauri ya Arusha na kuzifikia ya jumla ya kaya 9,107 kwa wamu ya kwanza na kaya 8,112, kwa awamu ya pili, huku kaya hizo zikipokea kiasi cha shilingi bilioni 9.5 kwa mizunguko 28 na jumla ya miradi 46 yenye thamani ya shilingi bilioni 2.1 ilitekelezwa katika sekta ya elimu, afya, miundombinu ya barabara, uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia vikundi vya kilimo, ufugaji na utunzaji wa mazingira.
ARUSHA DC
KaziInaendelea✍✍
PICHA ZA MATUKIO YA WAJUMBE WA KAMATI YA BUNGE IKIKAGUA MRADI WA KIKUNDI CHA KINAMA
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.