WASHIRIKI SHIMISEMITA ARUSHA DC WAASWA.
Arusha DC
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha ndugu Sulemani amefanya kikao na washiriki wa SHIMISEMITA watakao iwakilisha Halmashauri ya Arusha katika mashindano ya watumishi wa umma na Serikali za mitaa SHIMISEMITA yatakayofanyika Jiji Mwanza.
Akizungumza wakati wa kikao kilichofanyika katika ofisi ya Mkurugenzi amewataka washiriki hao kujiandaa kisaikolojia kwenda kushindana na siyo kushiriki.
Aidha, Msumi amewataka washiriki wote kuzingatia suala la nidhamu kipindi chote cha mashindano hayo.
"Mnapokwenda kushiriki tambuweni kwamba mnaiwakilisha Halmashauri yetu, wilaya na Mkoa kwa ujumla hivyo mnakila sababu ya kulinda heshima yetu kama watumishi wa umma" Amesema.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.