Na Elinipa Lupembe
Wasichana shule ya msingi Ilkiurei, halmashauri ya Arusha, wamepewa mashine ya kushonea nguo, (cherehani aina ya Butter fly) kutoka kwa wadau wa shirika lisilo la kiserikali la KUKUA PAMOJA TANZANIA, kwa ajili ya kushonea taulo za kike kwa wanafunzi wa shule hiyo, kujistiri wakati wa hedhi.
Wasichana hao wamepatiwa chereheni yenye thamani ya shilingi laki 3, ikiwa ni mradi wa kushona taulo zao za kike shuleni hapo, lengo likiwa ni kuhakikisha kila msichana anapata sodo awapo shuleni na kuweza kujistiri pamoja na kuhudhuria masomo kipindi chote cha masomo bila kipingamizi cha hedhi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mashine hiyo, mkurugenzi wa shirika la TUKUE PAMOJA Tanzania, Ayubu Patrick, amesema kuwa, shirika limefikia hatua hiyo, lengo likiwa ni kuwawezesha wasichana wasio na uwezo wa kupata taulo hizo wakati wa hedhi, ili asishindwe kuhudhuria masamo yao.
Ameeleza kuwa Shirika hilo kupitia mradi wa Tukue Pamoja, litawafundisha wasichana 20 kushona taulo hizo, na baadaye kuendelea kushona wenyewe huku wakiwafundisha wenzao na taulo hizo kugawiwa kwa wasichana wote shuleni ambao tayari wamefikia umri wa kuvunja unga.
"Tutakuwa na program ya kuwafundisha wasichana 20 kushona wakishaweza, watafundisha wenzao, lakini zaidi tutawafundisha elimu ya makuzi na mabadiliko ya kukua kimwili na athari zake pamoja na namna ya kujitunza katika hali za mabadiliko ya makuzi na ujana". Amesema Mkurugenzi Patrick.
Ameeleza kuwa takwimu zinaonyesha kuwa bado wasichana wanakabiliwa na changanoto ya kushindwa kuhudhuria masomo kwa kukosa vipindi 3 - 4 kwa mwezi na takribani vipindi 48 kwa mwaka wakati wa hedhi kwa kushindwa kumudu gharama za taulo za kike.
Hata hivyo wasichana hao, wamelishukuru shirika hilo kwa msaada huo, ambao wamethibitisha ni muhimu kwao, kwa kuwa wasichana wengi hushindwa kujiamini kipindi cha hedhi kutokana na kukosa uhakika wa kujisitiri.
Jemima James mwanafunzi wa darasa la IV, amebainisha kuwa ni kweli kuna tatizo la baadhi ya wasichana kushindwa kumudu kununua taulo za kike na baadhi kukosa masomo kipindi hicho cha hedhi, na kusababisha kuzorotesha maendeleo ya wasicha kimasomo.
"Kuna wasichana wakiwa kwenye hedhi, inawalazimu kuomba ruhusa na kubaki nyumbani, tukifundishwa kutengeneza sodo, itaturahisishia hedhi salama pamoja na kusoma kwa amani". Amesema Jemima
Naye Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ilkiurei, Mwl. Beatrice Kapinga, amesema kuwa wanafunzi wakiwa na uhakika wa kupata sodo shuleni, itaonheza ari ya wasichana kusoma kwa kuwa changamoto hiyo haitakuwepo tena.
ARUSHA DC
TUPO KAZINI ✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.