Wasimamizi wa wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata Wapewa Mafunzo ya siku 03 ya Kufuata Kanuni za Uchaguzi Kabla ya Uchaguzi wa Mkuu wa Rais ,Wabunge na Madiwani.
Wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya Kata wamepewa mafunzo yatakayohusu utekelezaji wa majukumu yao katika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uwazi, haki na amani.
Mafunzo hayo yamefanyika leo, Agosti 04, 2025, katika ukumbi wa mikutano wa Shule ya Sekondari Ilboru, Halmashauri ya Wilaya ya Arusha ,Washiriki walikuwa ni wasimamizi wa uchaguzi kutoka kata 27 za Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Akifungua mafunzo hayo, simamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Magharibi Stedvant Kileo , aliwataka wasimamizi wa uchaguzi kufuata kwa umakini miongozo na kanuni za uchaguzi ili kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unafanyika kwa ufanisi.
Aliwashauri wasimamizi hao kuwa makini katika majukumu yao na kuhakikisha kuwa kila hatua ya uchaguzi inatekelezwa kwa usahihi.
“Ni muhimu kwa wasimamizi m kufuata kila hatua ya miongozo na kanuni za uchaguzi, ili kuepuka dosari yoyote inayoweza kujitokeza. Hii ni hatua muhimu kwa ustawi wa demokrasia yetu na kwa ustawi wa jamii yetu,” alisema Msimamizi wa Uchaguzi Kileo.
Pia, Kileo alisisitiza umuhimu wa kudumisha amani na utulivu wakati wa uchaguzi, na aliwataka wasimamizi hao kutoa majibu bora kwa wapiga kura siku ya uchaguzi.
Aliwahimiza wasimamizi kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa mchakato wa uchaguzi unafanyika kwa amani, bila ya kuingiliwa na hali yoyote ya vurugu.
Mafunzo hayo yalifunguliwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha alisisitiza kwamba wasimamizi wa uchaguzi wanawajibika kwa usimamizi wa haki, uwazi na usalama wa wapiga kura.
Mafunzo yataendelea mpaka Agosti 06, 2025, huku lengo likiwa ni kuimarisha ufanisi wa wasimamizi wa uchaguzi na kuhakikisha uchaguzi Mkuu unafanyika kwa kuzingatia muongozo wa Kanuni za Uchaguzi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.