Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata, Jimbo la Arumeru Magharibi, wametakiwa kusimamia Kanuni, Sheria na taratibu za uchaguzi, kwa kutokujiingiza kwenye siasa, katika kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi mkuu, unaotegemea kufanyika tarwhe 28 Oktaba, 2020.
Rai hiyo iemetoewa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Magharibi, Saad Mtambule, wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya kata, mafunzo yanayofanyika kwenye ukumbi wa mikutana halmashauri ya Arusha.
Msimamizi huyo ngazi ya Jimbo, amewaasa Wasimamizi hao wasaidizi, kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia kanuni, taratibu na sheria zinazoelekezwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, taratibu ambazo zitawezesha kuwa na uchaguzi huru na wa haki katika shughuli zote wanazotakiwa kuzifanya kipindi chote cha uchaguzi mpaka kufika siku ya uchaguzi Mkuu.
"Tunalo jukumu kubwa la kuhakikisha uchaguzi unasimamiwa kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria za Uchaguzi, tumekula kiapo leo cha kutunza siri na kutokujihusisha na shughuli za chama chochote cha siasa, simamia kanuni bila kuyumbishwa na mtu yoyote" amesisitiza Msimamizi huyo wa Uchaguzi.
Naye Afisa Sheria Tume ya Taifa ya Uchaguzi Athmani Dunia, ameweka wazi kuwa mafunzo hayo ya siku tatu, yana lengo la kuwajengea uwezo wasimamizi hao, na kuwa na uelewa wa pamoja, juu ya kuratibu na kutekeleza majukumu ya uchaguzi mkuu, majukumu yaliyokasimiwa kwao na serikali kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Hata Mwenyekiti wa mafunzo na Msimamizi Msaidizi ngazi ya kata ya Nduruma, Loishuli Mollel, ameweka wazi kuwa wako tayari kupokea mafunzo, wanajiamini na wako tayari kupokea maelekezo tayari kwa kwenda kuyatekeleza majukumu hayo ya uchaguzi kwa mujibu wa kanuni, sheria n taratibu za uchaguzi mkuu.
Jumla ya wasimamizi wasaidizi 54 wa uchaguzi ngazi ya kata, kutoka kata 27 za Jimbo la Arumeru Magharibi, wameanza kupata mafunzo ya Uchaguzi Mkuu, mafunzo yaliyoambatana na watalamu hao kula kiapo cha kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi mkuu kuelekea tarehe 28 Oktoba, 2020.
PICHA ZA MATUKIO
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.