Na. Elinipa Lupembe.
Jumla ya wanafunzi 5,402, wanatarijia kuanza mitihani wa kidato cha IV kesho.Jumla ya watahiniwa 5,402 halmashauri ya Arusha, wilayani Arumeru, wanatarajia kuanza mitihani yao ya Taifa kesho Jumatatu, mitihani ya kuhitimu kidato cha nne mwaka 2021 kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Baraza la Taifa la Mtihani - NECTA.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Selemani Msumi, amesema kuwa, watahiniwa hao, watafanya mitihani hiyo kwenye shule za sekondari 48 za halmashauri hiyo, na kuwatakia watahiniwa wote kila la kheri katika mitihani yao na kuwataka kufanya mitihani yao kwa utulivu ili waweze kufaulu, kwa kuwa serikali imeshakamilisha taratibu zote kwa sehemu yake.
Pia amewasihi wasimamizi wote wa mitihani hiyo, kuepuka vitendo vya udanganyifu vitakavyosababisha uvunjifu wa sheria za mitihani ya Taifa, badala yake kuzingatia na kufuata kanuni, taratibu, Sheria na miongozo yote ya mitihani ya Taifa ikiwa ni pamoja na kuzingatia taratibu za watahiniwa wenye mahitaji maalum.
"Wasimamizi wote wamepewa semina elekezi, mafunzo yaliyowapa uwezo wa kuelewa taratibu zote za mitihani ya Taifa, wanafahamu 'do's na don't' katika usimamizi wa mitihani, serikali imewaamini na kuwapa dhamana hiyo kubwa kwa maslahi ya taifa letu, hivyo kila msimamizi akatekeleze wajibu wake kwa mujibu wa sheria". Amesitiza Mkurugenzi Msumi
Aidha mkurugenzi huyo, amethibitisha kuwa, maandalizi yamekamilika, na wanategemea kuanza mitihani hiyo kesho, kufuatia ratiba iliyotolewa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) na kuthibitisha kuwa watahiniwa wameandaliwa vizuri Kisaikolojia na wanategemea mitihani hiyo itafanyika kwa amani na utulivu.
Hata hivyo, Kaimu Afisa Elimu Sekondari, halmashauri ya Arusha, mwalimu Safi Mturi, amefafanua kuwa, watahiniwa watakaofanya mitihani hiyo ni pamoja na watahiniwa wa shule (School Canditates), watahiniwa wakujitegemea (Private Candidates) pamoja na watahiniwa wa Maarifa (QT).
Kaimu Afisa Elimu huyo, amefafaanua kuwa, idadi hiyo ya watahiniwa 5, 402, imejumuisha wa tahiniwa wa shule 4,988, ikiwa wavulana 2,061 wasichana 2,887, watahiniwa 398 ni wa kujitegemea huku watahiniwa 56 ni wale wa Maarifa - (QT).
Kaimu Afisa Elimu Safi, amethibitisha kukamilika kwa maandalizi yote kwa mujibu wa taratibu za mitihani ya Taifa, huku halmashauri ikiwa na mategemeo ya watahiniwa hao kupata matokeo mazuri, kutokana na maandalizi yaliyofanywa na walimu shuleni, sambamba na mkakati wa kutokomeza alama sifuri kwa watahiniwa wote wa kidato cha nne, 202.
Naye Mkuu wa shule ya sekondari Ilkiding'a mwalimu Supeet Sailevu, amethibitisha kukamilika kwa maandalizi yote katika shule yake kwa kuzingatia miongozo na taratibu zote, na kuongeza kuwa wanafunzi wa shule hiyo, wameandaliwa vizuri kisaikolojia, lakini pia wamefanya majaribio na mitihani mingi ambayo imewafanya kujiamini katika mitihani.
"Tunategemea wanafunzi wetu kupata matokeo mazuri, kwa kuwa kila mwalimu wa somo, amemaliza mada zote, na kuwandaa vema kwa mtihani huu wa Taifa, wanafunzi wamefanya mitihani mingi sana, kiasi cha kuwafanya wanafuzni wetu hawaogopi mitihani, iliyobaki tuwaombee tuu" amesema Mkuu huyo wa shule.
Halmashauri ya Arusha inawatakia watahiniwa wote, kila la Kheri katika mitihani yao, kufanya mitihani kwa amani na utulivu ili kupata matokeo mazuri.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.