Watalamu wasimamizi wa miradi ya BOOST halmashauri ya Arusha, wakifuatilia maendeleo ya utekelezaji wa madi wa ujenzi wa shule mpya ya msingi Kata ya Oldonyosambu.
Mradi unatekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 306.9 fedha kutoka Serikali Kuu kupitia Mradi wa Kuboresha Upatikanaji wa Fursa sawa katika Ujifunzaji Bora kwa Elimu ya Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST).
Mradi huu umejumuisha ujenzi wa jengo la utawala, vyumba vya madarasa 2 vya madarasa ya awali ya mfano, vyumba 7 vya madarasa ya shulenya msingi pamoja na matundu 16 ya vyoo.
Ikumbukwe kuwa, miradi hiyo ya ujenzi wa miundombinu shule za msingi ni utekelezaji wa Ilani ya CCM, Sura ya tatu Ibara ya 79 kifungu (q)Kukarabati miundombinu ya kufundishia na kujifunzia na kifungu (C)Kuboresha uratibu na usimamiaji wa stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.
ARUSHA DC NI YETU, TUSHIRIKIANE KUIJENGA
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.