Na. Elinipa Lupembe.
Watalamu watakaoshiriki kwenye zoezi la kitaifa la ukusanyaji na upangaji wa Anwani za Makazi, halmashauri ya Arusha, wametakiwa kufanya kazi hiyo kwa weledi na kuweka uzalendo mblele huku wakizingatia umuhimu wa zoezi hilo kwa maendeleo ya wananch na Taifa kwa ujumla.
Hayo yamesemwa Kaimu Mkurugenzi halmashauri ya Arusha, na Afisa Maendeleo ya Jamii, Angela Mvaa, wakati wa semina elekezi, iliyotolewa kwa watekelezaji wa zoezi la Anwani za Makazi wa kata ya Kiutu, semina iliyofanyika kwenye ofisi ya kata ya Kiutu.
Kaimu Mkurugenzi huyo, amewataka watalamu wote waliochaguliwa kutekeleza zoezi la upangaji wa Anwani za Makazi katika halmashauri ya Arusha, kuhakikisha wanatekeleza zoezi hilo kwa weledi kwa kuzingatia maelekezo, miongozo na taratibu walizopatiwa wakati wa mafunzo.
"Kila mshiriki wa zoezi hili anapaswa kutambua umuhimu wa zoezi hili kwa Taifa, na kutambua kuwa serikali imewaamini kuwapa kufanya kazi hiyo muhimj, hivyo mnapaswa kufanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa na kuhakikisha taarifa za wamiliki wa makazi yote zimeingia kwenye mfumo pamoja na makazi yote kupatiwa namba" amefafanua Kaimu Mkurugenzi huyo.
Aidha mafunzo hayo, yaliambata na mafunzo kwa vitendo ya namna ya kujaza taarifa za mmiliki wa makazi kwenye fomu maalum pamoja na namna ya kuandika na kubadika namba kwenye nyumba, ambapo Kaimu Mkurugenzi huyo alianza kwa kuandika nyumba namna 1 kwenye kitongoji cha Engorika kata ya Kiutu.
Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi huyo amewataka wananchi na wakazi wote wa halmashauri ya Arusha, kutoa ushirikiano watalamu na viongozi wa maeneo yao, watakaopita kwenye makazi yao kwa kuwapa taarifa sahihi zinazohitaji, lengo likiwa na kurahisisha zoezi pamoja na kukamilisha kwa wakati.
Naye Mratibu wa Anwani za Makazi, halmashauri ya Arusha, Loth Zachari ameweka wazi kuwa, mafunzo hayo, yenye lengo la kuwajengea uwezo watalamu wote wa ngazi ya kata, vijiji na vitongoji wataoshiriki katika utekelezaji wa zoezi hilo la Anwani za makazi, wakiwemo watalamu wa ngazi ya kata na vijiji, Maafisa watendaji wa kata na Vijiji, Wenyeviti wa vijiji na vitongoji pamoja na vijana waliopatiwa ajira za muda.
Mratibu huyo ameweka wazi kuwa, zoezi hilo linategemea kutekelezwa katika kata zote 27, vivijiji 67 na vitongoji 256 vya halmashauri ya Arusha na kuwataka wananchi wote kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa watalamu watakaopita kwenye Makazi yao kukusanya taarifa na kuandika namba kwenye nyumba zao.
ARUSHA DC
KaziInaendeleaa✍✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.