Na Elinipa Lupembe
Shirika lisilio la kiserikali la WaterAid Tanzania limetoa msaada wa taulo za kike 660, kwa wasichana wanaosoma shule za sekondari za pembezoni, halmashauri ya Arusha, lengo likiwa ni kuwapa wasichana uhakika wa hedhi salama isiyokuwa na vipingamizi na kuwapa uhakika wa kuhudhuria masomo kipindi chote cha masomo hata wakiwa kwenye hedhi.
Akizungumza wakati akigawa taulo hizo kwa maafisa Maendeleo ya Jamii wa kata, Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, Mhe. Ojung'u Salekwa, amelishukuru shirika kwa msaada huo muhimunkwa mtoto wa kike na kusisitiza kuwa kumuelimisha mtoto wa kike ni kuelimisha jamii, hivyo kuondoa changamoto kwa mtoto wa kike ni kuiondolea jamii changamoto.
Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi licha ya kuwashukuru wadau wa WatetAid, kwa kutambua thamani ya mtoto wa kike kwa kumuwezesha kujiamini wakati wa hedhi.
"Tunafahamu changamoto ni kubwa kwa watoto wa kike, hasa maeneo ya vijijini, wengi hukosa vifaa vya kujihifadhi na kulazimika kutokuhudhuria masomo, kwa msaada huu, WaterAid wamesaidia kupunguza tatizo hilo katika halmashauri yetu". Amefafanua Msumi.
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu, halmashauri ya Arusha, Angela Mvaa, amesema kuwa ugawaji wa taulo hizo utaenda sambamba na utoaji wa elimu ya kujitambua kwa wasichana ili kukabiliana na changamoto za kijamii, ikiwemo makuzi na mabadiliko ya mwili pamoja na athari za mahusiano ya kimapenzi katika umri mdogo.
"Tumeshuhudia vijana wanauana na wengine kujiua kwa ajili ya mahusino, hivyo tumeamua kuanza kuwapa elimu ya mahusiano na athari zake na namna ya kuishi katika mahusiano kwa kukabiliana na changamoto zake bila kuathiri uhai wa mwingine" . Amesisitiza Angela
Hata hivyo Afisa Elimu kata ya Bwawani, Mwl. Edward Mbesere, amethibitisha uwepo wa tatizo la wasichana kukosa taulo za kujihifadhi wakati wa hedhi na kusababisha kushindwa kuhudhuria masomo kila mwezi, kutokana na uwezo mdogo wa familia na kulifanya tukio hilo ni la siri miongoni mwa wanajamii.
"Mara nyingi msicha akisha vunja ungo, anaomba ruhusa ya kuumwa kila mwezi, ukifuatilia utagundua msichana hakufika shule kwa sababu yuko kwenye siku zake, na sio kwamba anaumwa ni kukosa vifaa vya kujistiri na kuamua kukaa nyumbani." Ameweka wazi Mwl. Mbesere
Awali shirika la WaterAid Tanzania limetoa jumla ya taulo za kike 660, ambazo zimegawiwa kwa shule za sekondari za Olokii, Musa, Sambasha, Oljoro, Losinoni, Losikito, Mukulat na Einotj zote zikiwa kwenye kata za mbali na miji.
ARUSHA DC
TUPO KAZINI✍✍
PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA MAKABIDHIANO YA TAULO ZA KIKE
Mwenyekiti halmashauri ya Arusha, Mhe. Ojung'u Salekwa, akimkabidhi taulo za kike, Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Lemanyata Nsia,
Marasa, kwa ajili ya kuzigawa kwa shuke ya sekondari Mukulat.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.